Ads

UWEKEZAJI UTT AMIS YAFIKIA SHILINGI TRILION 1.535

Na Francisco Peter, Dar es Salaam.

Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS imefanikiwa kupiga hatua kuwa katika ongezeko la mfuko hali ambayo imechangiwa na imani ya wawekezaji pomoja na elimu ambayo imekuwa ikitolewa  juu ya akiba na uwekezaji pamoja na faida shindani kwenye mifuko. 



Imeeleza kuwa utendaji wa mifuko umeendelea kuwa mzuri, faida kwa wawekezaji imekuwa kubwa ikilinganishwa na vigezo linganifu.

Kampuni ya hiyo ya Uwekezaji ya UTT AMIS  uwekezaji umeongezeka kutoka Bilioni 996.5 Katika kipindi Cha june 30/2022 hadi kufikia Shilingi Trion 1.535 katika kipindi june 30/2023.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam wakati wa mkutano mkuu wa mwaka wa wanahisa wa mfuko huo Mkurugenzi Mkuu wa ATT AMIS, Simoni Migangala amesema ongezeko hilo la Shilingi bilin 538.9 ni sawa na asilimia 54.0 ikilinganishwa na ongezeko la shilingi bilion 383.7.

"Ongezeko la ukubwa wa mifuko linatokana na imani ya wawekezaji kwetu ,elimu itolewayo juu ya akiba na uwekezaji pamoja na faida shindani kwenye mifuko. Utendaji wa mifuko kwa kwa kipindi hicho umeendelea kuwa mzuri, faida kwa wawekezaji ilikuwa kubwa ikilinganishwa na vigezo linganifu". Amesema Migangala na kuongeza kuwa 

"Faida kwa mwaka kwa upande wa mifuko inayowekezwa kwenye hisa na maeneo yenye mapato ya kudumu ni kama ifwatavyo, mfuko wa umoja Asilimia 11.2%,mfuko wa wekeza maisha asilimia 12.5% ,mfuko wa watoto asilimia 12.4% ,mfuko wa jikimu asilimia 14.0% ikilinganishwa na asilimia 7.6% ya kigezo linganifu". 

Ameongeza kuwa kwa mifuko iliosalia yenye uwekezaji kwenye maeneo yene mapato ya kudumu faida kwa mfuko wa ukwasi ni asilimia 12.5% na mfuko wa hatifungani ni asilimia 12.3% ilinganishwa na asilimia 9.7 ya kigezo linganifu.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya UTT AMIS ameishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira bora ya Uwekezaji hali iliyosababisha ongezeko la ukuaji wa masoko ya fedha nchini yaliyochangia kuendelea kukua wa UTT AMIS.

Ameongeza kuwa UTT AMIS inamipango mikubwa ikiwemo kuangalia namna ya kuingia katika masoko ya Afrika Mashariki baada ya kufanya vizuri hapa nchini.

No comments