Ads

Waziri Dkt. Ashantu Amwagia Sifa NDC Umiliki Mradi Mkakati :Ni Mchuchuma na Liganga Utakaochochea Fedha za Kigeni

Na Francisco Peter

Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt.Ashantu Kijaji amempongeza Mkurugenzi wa  Shirika la Taifa la Maendeleo nchini (NDC)Dkt.Nicolaus Shombe kwani serikali kupitia shirika hilo imekuwa na dhamira ya kuhakikisha ndoto za utekelezaji  wa mradi wa Liganga na Mchuchuma zinatimia.

Serikali imeweza kutoa kongole kwa (NDC) kwa kuwa imekuwa ikimiliki maeneo ya miradi ya kimkakati  huku ukitajwa kuwa wakati umefika kwa rasilimali iliyopo katika miradi ya makaa ya mawe ya Liganga na Mchuchuma kuanza uzalishaji na kuwa makaa hayo yanaitajika sana nje ya nchi hali italayochochea upatikanaji wa ajira na kuongezeka kwa fedha za kigeni.

 Hayo yamebainishwa na Waziri wa Viwanda na Biashara,Dkt.Ashantu  jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya utiaji saini wa Mikataba ya Uchimbaji wa  Makaa ya Mawe kwa wachimbaji wazawa katika mradi huo ,  baina ya Serikali kupitia Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) pamoja na Makampuni matano ya wazawa yaliyoshinda zabuni hiyo.


"Ni dhamira ya dhati na ya hali ya juu ya serikali kuhakilisha ndoto za utekelezaji wa mradi wa Liganga na Mchuchuma Sasa zinatimia na rasilimali hizi ambazo zimekaa kwa muda mrefu bila kuwanufaisha wananchi ziwanifaishe na  kuchangia katika uchumi wa nchi," Amesisitiza Dkt.Ashatu.

Dkt.Ashatu amesema makampuni hayo yanatarajiwa kizalisha jumla ya tani 1,800,000 kwa  mwaka .

Amesema serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itakuwa imechangia mafanikio hayo , imetoa kiasi cha Shilingi bilioni 15.4 za kitanzania ikiwa ni malipo ya fidia kwa wanufaika 1,142 ambao watapisha utekelezaji wa mradi huo.


Dkt. Ashatu amesema imekuwa ni shauku kuona mradi huu wa muda mrefu unatekelezwa kwa kuanza uzalishaji na amempongeza  Rais Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuboresha mazingira ya biashara na kuifungua Tanzania kiuchumi na hivyo kuvutia uwekezajo wenye tija katika nchi yetu.

Pia alibainisha kuwa wafidiwa wote waliokuwa na wasiwasi kuhusu uhalisia  wa fidia zao walihakikiwa upya maeneo ya ilikuhakikisha hakuna malalamiko ambayo hayakutafutiwa ufumbuzi huku kila mnufaika akiwa amepata stahiki zake kama ilivyo ainishwa katika ripoti ya tathmini.

Hata hivyo utekelezaji wa malipo hayo umeelezwa kuwa ulitokana na ahadi iliyotolewa mwaka 2020 katika kampeni za uchagizi mkuu ambapo Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati huo akiwa mgombea mwenza  wa nafasi ya Makamu wa Rais aliahidi kulipa fidia kwa wananchi hao.

Wakato huo huo imetajwa pia kwa ujumla zoezi la fidia limefanyika kwa mafanikio makubwa huku watu 25 tu kati ya wafidiwa  1142 ndio hawajapokea fidia kutokana na kujitokeza ili kujaza nyaraka za malipo.

"Uongozi wa Wilaya ya Ludewa na vijiji vyao unawasiliana na wahusika ili wanaostahili waweze kukamilisha taratibu na hatimaye kulopwa fidia zao," amesema Dkt. Ashatu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa NDC , Dkt.Nicolaus Shombe amesema awali mchakato huo unulihusisha jumla ya Kampuni ishirini na tano (25) ambapo jumla ya kampuni 17 zilifanikiwa kuwasilisha maombi yao kwa ajili ya uchambuzi na ushindani na hatimaye zilipatikana zilipatikana kampuni Tano zilizokidhi vigezo.

Aidha amesema leo hii yanakodishwa vitalu katika awamu ya kwanza ya mradi huo , huku NDC ikitaja kupatikana kwa zaidi ya uitaji wa ndani ya nchi kuwa ni mzuri kuchochea maendeleo.


"Kampuni hizo ishirini na Tano zilipewa nyaraka za  zabuni kupitia mfumo wa ununuzi serikalini (TANePs) ambapo kampuni 17 zilifanikiwa kuwasilisha nyaraka za zabuni,"alisema Dkt.Shombe.

Dkt. Shombe alieleza kuwa mradi huo utakiwa na manufaa makubwa kouchumi ikiwemo kutoa ajira zaidi ya mia Tano za moja kwa Moja , kurahisisha upatikanaji  wa nishati inayotokana na makaa ya mawe kwa viwanda jambo litakalo chochea ukuaji wa viwanda nchini pamoja na kuingiza fedha za kigeni kwa mkaa utakao uzwa nje ya nchi hususan nchi jirani.

Kufuatia mkakati huo jumla ya kampuni  hizo Tano zilizo tiasaini katika mradi huo ni Sheby Mix Investment Limited , Nipo Engineering Company Limited ,Chusa Mining Company Limited .

Baadhi ya kampuni nyingine ni Kindaini Company Limited na Cleveland Mine and Service Company Limited ambapo mkayaba huo umetajwa kudumu kwa miaka mitano.

Waziri Dkt. Ashantu  Amwagia Sifa NDC Umiliki Mradi Mkakati :Ni Mchuchuma na Liganga Utakaochochea Fedha za Kigeni 

No comments