MKURUGENZI WA JIJI DSM APONGEZA UTENDAJI WA MENEJA MPYA SOKO LA FERI
Na Francisco Peter, Dar es Salaam
Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam inayoongwazwa na Mkurugenzi Jomaary Mrisho amepongeza hatua za makusanyo ya ushuru katika miezi michache tangu alipoanza kazi Meneja mpya katika Soko la Kimataifa la Samaki Feri lililoko Kivukoni Dar es Salaam .
Meneja huyo mpya katika Soko hilo Seleman Mfinanga tayari ameonekana kupewa kongole katika utekelezaji wa shughuli hizo za Soko hilo kufuatia kukuza kupandisha malengo ya ukusanyaji mkubwa wa mapato ya serikali.
"Ni kweli mapato katika ukusanyaji wa kodi yameweza kupanda hivyo ni hatua nzuri kwani wakati nampeleka hapo niliamini nimepeleka mtu sahihi wa kuweza kufanya kazi ,"amesema Mrisho.
Kwa upande wake meneja huyo wa Soko la Kimataifa Feri Mfinanga amesema amekuwa akitatua kero zinazojitokeza kwa haraka ambapo hatua hiyo imeonesha kusaidia kupandisha mapato ya serikali kwa haraka.
Amesema soko hilo limekuwa likijiendesha kupitia mapato wanayokusanywa , ambapo tayari kwa muda mfupi ameweza kuvuka malengo .
"Nimeweza kuvuka malengo yaliyopangwa na serikali , tumeweza kuyavuka kimapato katika muda mchache ,".
"Ninaangalia na kujiwekea malengo ya kukusanya kila mwezi tukusanye kiasi gani, hivyo tunahakikisha pia kila mwisho wa mwezi tunapeleka asilimia 30 ya mapato katika halmashauri kwa ajili ya shughuli za maendeleo," amesema Mfinanga.
Amesema Soko hilo la Kivukonii Jijini Dar es Salaam linakabiliwa na changamoto ya kuwa na idadi kubwa ya wafanyabiashara zaidi ya 3000 huku uwezo wake halisia ni kuwa na uwezo wa kuhudumia wafanyabiashara wapatao 1500.
Akizungumza hilo katika mahojiano maalumu na mtandao huu hivi karibuni Mfinanga amesema kuwa kuongezeka kwa wafanyabiashara hao kunachangia kuharibika kwa miundombinu ya soko hilo mara kwa mara na hivyo amekuwa akitatua kero ndogo ndogo kwa haraka.
Amesema mpango wa Serikali ya Awamu ya Sita ya Dkt.Samia Suluhu Hassan ni kuondoa adha inayojitokeza kwenye masoko hali inayofanya uongozi wa soko hilo kuwa na mikakati mizuri ya kuhakikisha wafanyabiashara hao wananufaika katika kujiingizia kipato na serikali kunufaika na kodi katika kufanya shughuli za kimaendeleo.
Sanjari na hayo amesema kutokana na kuwepo kwa idadi kubwa ya wafanyabishara lakini wanaendelea kujitahidi kuhakikisha suala la usafi wa soko unafanyika ipasavyo ili kuzuia Magonjwa ya mlipuko ambapo taka za maeneo hayo zimekuwa zikiondolewa kwa wakati.
Hata hivyo Meneja wa Soko hilo ameahidi kufanyia kazi changamoto endapo zitaendelea kujitokeza huku akiwataka Wafanyabiashara wa soko hilo kuendelea kufanya kazi kwa bidii huku wakitambua kuwa Serikali ipo nyuma yao na inahakikisha inawatengenezea mazingira mazuri yakufanyia biashara.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo ameweza kuwa anajibu changamoto mbali mbali za kuhakikisha wanaimarisha ulinzi na usalama wa soko lakini pia kuboresha vyanzo vya ukusanyaji mapato ili kuzuia upotevu wa fedha zitokanazo na soko .
"Nampongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam pamoja na uongozi wa Soko la Kimataifa la Feri kwakuweza kufanya kazi nzuri za utendaji lakini pia nawapongeza wafanyabiashara kwa kulipa kodi kwani kwa kufanya hivyo inaongeza pato la taifa kwa asilimia kubwa." Amesema Mhe. Mpogo alipo kuwa as kifanya hatua mbali mbali za ziara katika soko hilo.
Post a Comment