WATISHIA KURUDISHA KADI ZA CCM KISA KUTOLEWA LUGHA YA MATUSI NA KIONGOZI WA SERIKALI ,WAKINYANGA'WA SOKO.
Baadi ya wazee na viongozi wa wafanyabishara ndondogo Soko la Mabibo ambao pi ni wanancha wa Chama cha Mapinduzi CCM wakizungumza na waandishi wa habari , Picha na Mpigapicha wetu
Baadi ya wazee na viongozi wa wafanyabishara ndondogo Soko la Mabibo ambao pi ni wanancha wa Chama cha Mapinduzi CCM wakizungumza na waandishi wa habari , Picha na Mpigapicha wetu
Baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi CCM Katika soko la Ndizi Mabibo wametishia kurudisha kadi za Chama hicho ikiwa hawatasikilizwa na kutatuliwa mgogoro wa Soko lao Maarufu Mahakama ya Ndizi.
Wanachama hao wamejitokeza mbele ya vyombo vya habari wakidai kuwa Soko hilo lilikabidhiwa kwa wafanyabisha na Rais wa awamu ya Tano hayati Dakta John Pombe Magufuli 13/10/2020.
Akizungumza kwa niaba ya Wazee ambao amesema wamefedheheshshwa na kitendo matumizi ya Lugha ya matusi kutoka kwa kiongozi wa Serikali Mmoja wa waanzikishi wa Soko hilo Rashid Mohamed Kala alisema
''Sisi wafanyabishara ndondogo hapa Sokoni tupo takribani elfu kumi la wanachama wa CCM tupo takribani elfu Sita ,suala la kurudisha kadi halitupendezi nidiyo maana tumejitikeza kwenu waandishi wa habari Ili ujumbe ufike kwa Mwenyekiti wetu Taifa kwamba ikiwa hatutasikikizwa hatunabudi kufanya hiyo "aliongea kwa uchungu mmoja wa wanachama hao ambeye alisema kuwa yeye ni mwanachama kuanzia TANU na baadaye CCM huku akionesha kadi yake ya uanacha ile ya kielectronic.
Alisema yeye pamoja na Wazee wote wenye umri mkubwa alifedheheshwa Sana na kauli iliyotumiwa na Mkuu wa mkoa wakati alipofika Sokoni hapo kutaifisha Soko kwani hakutumia Lugha ya staha kwa kusema
"Mkome kama mlivyo koma maziwa kwa Mama zenu wapumbavu Sana ninyi kama kunamtuanabisha askari weka kwanye karandinga "
Sasa wengine niwatu wazima Mimi hapa nina miaka 72 huyu nikama Mwanangu ama mdogo wangu kwanini atutukane?
Walisema kwa wanachofahamu nikwamba mwenye mamlaka ya kutengua uamuzi wa mkuu wa nchi ni Mkuu wa nchi na si mkuu wa mkoa Wala kiongozi mwingine wakidai kuwa maamuzi yaliyofanywa na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam mwezi Agosti 2023 ni batili.
''Mkuu wa Mkoa aliyepita Amos Makala alipotembelea kusikilza kero za wafanyabiashara alisema hawezi kuitengua amri iliyowekwa na Rais na alikuja kwa Lugha nzuri sasa huyo hatujui ametumia kigezo gani ''
Akizingumza kuhusu uatarabibu wa Soko hilo Mwenyekiti wa masoko Mwenyekiti wa Vibindo Society Tanzania (Chama mwamvulincha wafanyabishara ndondogo Tanzania) Gaston Kikuyi kwa niaba ya wafanyabishara ndondogo Soko la Ndizi Mabibo amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kuingilia Kati kwani utaratibu uliotumiwa kunywngang'a Soko hilo haukuwa shirikishi badala yake limechukulia kwa mabavu.
"Tunamuomna Rais Dakta Samia Suluhu Hassan aingile Kati suala hili kwakuwa sisi hili Soko tuli kabidhi na Rais wa awamu ya Tano na tulikuwa tunaliendesha vizuri na Serikali inafahamu kwamba tuna mpango wa kulijenga na usanifu tumeshafanya tumeshaanza kuingia gharama "Alisema
Wameendelea kusema kuwa eneo la Soko hilo walivamia ila wamiliki halali ni Kiwanada Cha nguo Cha URAFIKI walikuta eneo hilo halitumiki ni chafu na kulikuwa na nyoka na wadudu wakali wa Kila namna na kulikuwa kunajaa maji wakachangishana na kujaza kifusi anagalau wakaweza kupanga biashara zao.
"Pamoja na kwamba tulivamia baadaye tulifanya mazungumzo na wamiliki wa eneo tukawa tunawalipa hivyo hatukukaa Bure na baadaye Manispaa ya Kinondoni wakati huo haijagawanywa kuwa Ubungo nao wakaja tukafanya nao mazungumzo tukawa tuna walipa million Sita Kila mwezi na hata ungozimpya wa Wilaya ya Ubungo tukaendelea kuwalipa mpaka hapo mwaka 2020 oktoba tulipo kabidhiwa na Rais kwa maelekezo kwamba tuboreshe na kulihudumia Sokonkwa gharama bili za Umeme maji na miundo mbinu "Alisema
Mimi ni mjumbe wa Baraza la biashara Taifa nafahamu Serikali inataka ushirikiano na sekta binafsi na malanyingi Rais Samia amekuwa akisisitizo hilo na Mimi nilipata fursa ya kushiriki mkutano wa Sektabinafsi na Serikali tarehe 26 Juni 2022 ,Niliwasilisha wazo kuhusu eneo hilo la Soko kwamba lipimwe limilikishwe kwa wafanyabishara ndogondogo tulimiliki maana kimsingi hata kiwanda Cha nguo hivi Sasa hakitumii eneo hilo na shughuli hazifanyiki badala yake limekuwa vituo vya magari na biashara zingine.
Kutokana na kwamba Mhe .Rais anapenda Sekta binafsi katika taarifa yake aliridhia kwamba eneo hilo lipimwe na aliye pewa kazi hiyo ni wizara ya Ardhi walipima eneo hilo Lina ukubwa wa square mita 3889, kwahiyo kutokana na mapendekezo ya ule mpango kupitia hazina nikwamba serikali inajadiliana na Kiwanda Cha Urafiki
Post a Comment