Ads

Serikali Yakazia Dawa za Kuua Viluwiluwi wa Mbu nakuwa Imefikia Nchi Saba Afrika

Na Francisco Peter 

WAZIRI wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji ametembelea kiwanda cha dawa za kuua viluwiluwi wa Mbu (TBPL) kilichopo Kibaha mkoani Pwani 



na kuwa kimekuwa na mpango mkakati wa kupata masoko ya nje na ndani na pia kuanzia kuzalisha bidhaa za Viuatilifu hai kwa ajili ya Kilimo.

Dkt. Kijaji ametoa kauli hiyo Jana Septemba 21, 2023 wakati akizungumza na Uongozi, Watumishi na waandishi wa habari baada ya kufanya ziara kiwandani hapo kuona maendeleo yake.

“Bidhaa nyingine ni viuatilifu hai, bidhaa inayotumika kwa ajili ya afya ya mimea na tarehe tarehe 21/6/2023 mamlaka ilitupatia usajili wa bidhaa hii, hivyo tunakwenza kwa wingi,” amesema Dkt. Kijaji na kuongeza,

“Na ningependa bidhaa hii Mwezi wa 10 Mwaka huu ianze kuzalishwa kwa wingi na iingie sokoni kwani huu ni msimu wa Kilimo,”.

Amesema kiwanda hicho kimeweza kuuza dawa hiyo katika nchi za nje zikiwemo Angola,Botswana, Uganda kwa kuwa kwa sasa nchi yetu ipo kwenye soko la ubora kwenye soko huru Afrika.

Ameagiza kuhakikisha dawa hiyo inawafikia wakulima na kueleza kuwa haina kemikali na kwamba inawekwa kwenye mmea wa aina yoyote na haina madhara.

Ameeleza kuwa dawa hiyo ni rafiki kwa Mazingira, afya ya Binadamu na mimea.

Waziri wa Viwanda Dkt. Kijaji amesema kwamba atamuomba Waziri wa Kilimo Hussein Bashe kuhakikisha Vijana ambao wapo katika Mradi wa Kilimo wa BBI wanatumia bidhaa hiyo.

“Bidhaa hii ni bora, haina madhara, lengo ni kuhakikisha tunazalisha bidhaa bora,” amesema Dkt. Kijaji.

Ametumia fursa hiyo kuupongeza uongozi wa kiwanda hicho kwa kutekeleza maagizo aliyotoa alipotembelea kiwanda hicho.

Amesema kuwa dawa ya viluwiluwi vya kuua Mbu inayozalishwa na kiwanda imekubaliwa barani Afrika ambapo hadi sasa imefikia Nchi saba, ambazo miongoni mwake ni Kenya, Angola, Botwana, Msumbiji Niger na hivi karibuni itaanza kupelekwa nchini Uganda.

Hata hivyo ameagiza uongoza kuendelea kutafuta masoko ya bidhaa za kiwanda hicho ndani na nje, pamoja na kuboresha kitengo cha masoko.

Kwa pande wake Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) Dkt. Nicolas Shombe ameeleza kuwa kiwanda hicho kinazalisha bidhaa za kibaolojia za kuulia viluwiluwi vya Mbu.

Amesema kuwa kiwanda hicho ni cha kipekee na cha Kimataifa kwamba pamoja na kuazalisha sawa hiyo ya viluwiluwi wa mbo lakini pia ni maabara kubwa bidhaa za kibaolojia.

No comments