UTALII NDANI YA HIFADHI YA NGORONGORO
Na Francisco Peter
Kampuni ya Wellworth Hotels and Lodges Ltd inayomiliki hoteli zake nchi , inaonesha kuwa na wafanya kazi wengi wazawa katika hotel ya Ngorogoro Oldean Mountain Lodge .
Wakati huu juhudi kubwa za kuzungumzia mazuri yaliyoko katika sekta ya Utalii nchini duru za kisekta zinaonesha yapo mambo mazuri ya kusifia ukuwaji katika huduma wanayopata watalii wa ndani na wanaotoka nje ya nchi.
Hifadhi ya Ngorongoro (Ngorongoro Conservation Area) ni hifadhi ya taifa kaskazini mwa Tanzania inayojulikana kote duniani, hasa baada ya kuorodheshwa na UNESCO kati ya mahali pa Urithi wa Dunia ambapo umbali wa takriban kilomita 180 kutoka Arusha."Kunajumla ya wanyamapori wakubwa takriban wakiwa pamoja na vifaru, viboko, nyumbu, pun
Willy anasema hoteli hiyo inajumla ya wafanyakazi 100 huku asilimia 95 ikiwa ni wazawa hali inayochochea sana ajira za watanzania wazawa kujiingizia kipato na serikali kipata kodi yake .
"Tunazo heka zisizo pungua 50 katika eneo hili likiwa limepandwa miti ya kuvutia ndege nyingi , wapo ndege wasio pungua 150 hali inayofanya waonekane kila kona ,"anasema Willy.
Anasema eneo limezungukwa na bara bara ambapo mgeni pia anaweza kufanya mazoezi kwa kutumia njia hizo huku eneo lote likiwa na uzio mzuri pamoja na bwawa la kuogelea lenye kina kidogo.
Pia gorogoro Oldean Mountain Lodge inaelezwa kuwa inanarestaurant Lodge , baa ,Gym mambo mengine ni pamoja na kuwepo chumba cha watoto (Kids Club) ambapo mtoto anaweza kicheza pengine mzazi akiendelea na shughuli zake.
"Lodge inavyumba 51 ila chumba kimoja ni Cha kipekee kabisa kikiwa ni cha watu wenye hadhi , vyumba 50 ni vyumba vinavyo fanana vyote ," anamalizia kusema Willy.
Kwa upande wake Emanuel Mayo kutoka kampuni ya Shingondefu Safaris ambayo ni kampuni yenye ushindani katika kupeleka wageni kwenye hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro anasema hifadhi inawanyama zaidi ya elfu 20 huku nusu ya wanyama hao ikiwa ni nyumbu .
"Kuna familia ya Simba ambazo zipo Tano hadi familia Nane huku familia moja ikiweza kuwa na Simba 20 hadi 50 as mbapo wanaonekana kwa macho kwenye eneo la bonde pekee,"anasema Mayo huku akieleza kuwa Nyumbu ni wanakadiliwa kuwa elfu kumi na zaidi huku akitaja blonde lina kilomita 1700 kutoka usawa wa bahari.
Awali akizungumza Mkurugenzi wa Kampuni Tanzu ya Wellworth Hotels and Lodges Ltd Zulfikar Ismail amesema kwamba kampuni hiyo inamilikiwa na Watanzania kwa asilimia mia moja na ndani ya miaka miwili ijayo wanatarajia kuwekeze jumla ya hotel 22 Tanzania nzima.
Ambapo hivyo anafurahishwa na juhudi za serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuendelea kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji wazawa.
Nae Afisa Masoko wa Kampuni hiyo Josephine Makundi amekuwa haki sisi tiza kwamba hotel na lodges zote za kampuni hiyo zinauwezo wa kuwahudumia wateja wanaolala zaidi ya elfu moja kwa siku Moja.
Kampuni ya Wellworth Hotels and Lodges inamiliki hotel ya Ngorogoro Oldean Mountain Lodge,Lake Manyara Kilimamoja Lodge,Tarangire Kuro Treetops Lodge,Ole serai Luxury Camp -Moru Kopjes,Ole serai Luxury Camp- Turner Springs,Ole serai Luxury Camp- Kogatende,Ole serai Luxury Camp- Seronera,Kunduchi Wet n Wild Waterpark.
Post a Comment