TCB YAIPIGATAFU SHULE YA MSINGI KIKELELWA MKOANI KILIMANJARO.
Mkurugenzi wa hazina. Wanceslaus Fungamtama akizindua matundu ya vyoo katika shule ya msingi kikelelwa halmashauri ya Wilaya ya Rombo mkoani kilimanjaro mwishoni mwawiki ujenzi huo umedhaminiwa na Benki ya TCB wapili kulia ni mkuu wakitengo cha mawasiliano katika benki hio. Chichi Banda. na viongozi wengine wa shule na ofisi hiyo. Nampiga picha wetu
Mkurugenzi wa Hazina akikagua Matundu ya vyoo baada ya kukata utepe akiwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Bi. Chichi Banda mwishoni mwa wiki wilaya ya Rombo.Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kikelelwa wakifurahia matumizi ya majengo yaliyojengwa chini ya ufadhili wa TCB Baada.
Mwamba wa habari
Zaidi ya wanafunzi 700 katika shule ya msingi Kikelelwa iliyopo wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro ambao walikuwa hatarini kupata magonjwa ya mbalimbali kutokana na vyoo walivyokuwa wanatumia awali kuwa chakavu na vyenye matundu machache wameondokana na changamoto hiyo baada ya benki ya Taifa ya kibiashara (TCB) kujenga matundu ya vyoo kumi na nane(18).
Akizundua vyoo hivyo shuleni hapo mkurugenzi wa Hazina Tanzania Commacial Bank Wenceslaus Fungamtama kwa niaba ya Afisa mtendaji mkuu wa benki hiyo, Sabasaba Moshingi amesema lengo la kujenga vyoo hivyo ni ili kuboresha mazingira na utulivu wa kujifunza kwa wanafunzi hao wawapo shuleni.
"Ili kuunga jitihada za serikali za kuboresha huduma za kijamii ikiwemo afya na elimu, benki ya TCB hutenga kiasi cha zaidi ya milioni milioni 300 kila mwaka ambapo kwa mwaka huu zimeweza kujenga madarasa, nyumba za walimu na vyoo katika maeneo mbali hapa nchini" amesema Fungamtama.
Mwalimu mkuu wa shule hiyo Charles Amos amesema kutokana na uchache wa matundu ya vyoo yaliyokuwepo awali wanafunzi walilazimika kupanga foleni ya kusubiriana huku wale wadogo kujikojolea.
"Tunawatoto waliokuwa wanatoroka kwenda nyumbana kwa aibu ya kujikojolea, hasa muda wa mapumziko ambao wanatoka darasani kwa pamoja, lakini sasa kwa vyoo hivi ni wazi kutakuwa na utulivu wa kujifunza" amefafanua Mwl.Amos
Dada mkuu wa shule hiyo Careen Jonas ameonyesha furaha yake kuwa licha ya vyoo hivyo kujengwa kisasa, vikizingatia miundombinu ya walemavu lakini pia vina chumba maalumu cha kubadilishia nguo kwa waschana wawapo kwenye siku zao za hedhi.
Kwa upande wake Afisa elimu idara ya elimu msingi halmashauri ya wilaya ya Rombo Alice Makule, amesema hivi sasa shule inajumla ya wanafunzi 768, wavulana 385 na waschana 378 ambapo kwa uwiano ilitakiwa kuwe na matundu 16 kwa wavulana na 19 kwa waschana lakini wakitumia matano matano tu hivyo ujio wa benki hiyo kujenga matundu 18 umepunguza tatizo kwa kiasi kikubwa.
Shule ya msingi Kikelerwa ambayo ipo mpakani mwa Tanzania ni moja kati ya shule kongwe za mkoa wa Kilimanjaro, licha ya kukabiliwa na changamoto lukuki ikiwemo uchakavu wa madara, vyoo na uchache wa walimu lakini imeelezwa kufanya vizuri kiufaulu.
Post a Comment