Mamlaka ya mafunzo ya amali Zanzibar yaweka wazi mipango ya kumkomboa kijana kiuchumi.
MAMLAKA ya Mafunzo ya amali Zanzibar VTA imesema Katika mipango yake ya kuwaendeleza vijana kujipatia ujuzi na ufundi imekusudia kujenga vyuo 6 Kila wilaya visiwani humo.
Katika vyuo hivyo kimoja kitakuwa kinatoa Mafunzo yanayoendana na uchumi wa Buluu kama vile Ubaharia,ufundi wa vyombo vya Baharini,Mafuta na Gesi ukulima na usarifu wa Mwani .
Hayo yamebainishwa na kaimu afisa uhusiano wa mamlaka ya Mafunzo ya amali Zanzibar Tawhida Shabani Jabu Katika Maonesho ya 47 ya biashara ya kimataifa Sabasaba jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mamlaka hiyo.
Amesema kujengwa kwa vyuo hivyo vitawasaidia vijana kupata Mafunzo ya amali bila usumbufu wa kutembea umbali mrefu kufuata masomo na kuongeza idadi ya vijana wenye ujuzi na kukabiliana na tatizo ajira.
"Nawashari na ninawaita vijana wazidi kuchangamkia fursa waje kujiunga na Mafunzo haya kwa sababu wanapo maliza Mafunzo huwa tunawapa mikopo nafuu isiyo kuwa na riba "Alisema.
Amesema namna ya kupata mikopo hiyo ni vijana kujiunga Katika vikundi vya kuanzia watu watano wafani Moja walio soma Katika vyuo vya amali.
Pamoja na hayo amesema Katika kuunga mkono Sera ya serikali kukuza uchumi wa Buluu wabunifu Katika vyuo vya Mafunzo ya amali wamebuni Mashine mbalimbali ikiwemo Mashine ya kuchakata mwani.
"Vijana wetu pia Katika faninnyingine wamebuni Mashine ya kukaushia nguo, na Mashine ya kutolesha vifaranga" Alisema
Mamlaka ya Mafunzo ya amali Zanzibar kupitia vyuo vyake vitano vilivyopo Unguja na Pemba inatoa mafunzo Katika fani 21, na vyo vyake vinapokea vijana kutoka pande zote za Muungano.
Kwa Maelezo zaidi tembelea Banda lao Katika Maonesho ya 47 ya biashara ya kimataifa Sabasaba Banda la Zanzibar au fika Katika ofisi za vyuo vya Mafunzo ya amali vilivyoko Unguja na Pemba.
Lengo kuu la kuanzishwa mamlaka ya amali ni kukuza taaluma na ujuzi kwa vijana kwa kuwapatia Mafunzo ya elimu ya ufundi itakayo waweke Katika nafasi ya kuweza kuajiriwa serikalini ,sektabinafsi na kujiajiri wenyewe.
Post a Comment