TUME YA USHINDANI FCC YAWEKA WAZI MIPANGO YAKE YA KUTOA ELIMU KWA WANANCHI.
Mwenyekiti wa Bodi ya tume ya ushindani FCC Dakta Aggrey Mlimuka akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa FCC alipotembelea banda la tume hiyo katika maonesho ya 47 ya biashara ya kimataifa sabasaba jijini Dar es salaam.
Mwamba wa habari.
Mwenyekiti wa Bodi ya tume ya ushindani FCC Dakta Aggrey Mlimuka ametoa wito kwa watanzania kutoa taarifa kwa tume ya ushindani iwapo wataona kuna bidhaa ambazo wanazitilia shaka kuwa ni bandia.
Dakta Mlimuka ameyasemahayo Katika banda la Tume hiyo Katika Maonesho ya biashara ya 47 ya biashara yanayoendelea jijini Dar es salaam.
Aidha amesema Tume hiyo Katika kipindi Cha mwaka mmoja imepiga hatua kwa kufungua ofisi tatu za Kanda hapa nchini.
"Nimefaraijika kuona wafanyakazi wa tume wanaendelea kutoa elimu Katika banda letu na kwamba tumepiga hatua ukilinganisha na mwaka Jana kipindi kama hiki tulikuwa na ofisi Moja tu Dar es salaam,Sasa tuna ofisi Arusha ,Mwanza na Mbeya.
Katika hatua nyingine Dakta Mlimuka amewataka wananchi na wafanyabiashara wanaotaka kuwa na muunganiko kibiashara unaoanzia shilingi bilioni tatu kufika Katika ofisi za tume hiyo Ili muunganiko huo upate nguvu ya kisheria.
Pamoja na hayo Katika kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu ushindani amewakumbusha wananchi kuwa kunasiku maalumu ambazo zimetengwa kitaifa ambazo ni siku ya mtumiaji ambayo hufanyika Kila mwezi marchi na siku ya bidhaa bandia ambayo hufanyika Juni 13 ya Kila mwaka.
Post a Comment