CHUO KIKUU CHA TAIFA CHA ZANZIBAR KINAVYOWAJENGA WANAFUNZI KUJIAJIRI
Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kimewataka wazazi na walezi waweze kuwapatia watoto wao elimu bora pamoja na maarifa yatakayo wawezesha kujiajiri wenyewe wanapomaliza masomo yao chuoni.
Dkt. Ahmed amesema kuwa wanafunzi wa Chuo wamekuwa wakijifunza kwa vitendo pamoja na kutengeneza bidhaa mbalimbali kwa kutumia mimea.
"Hii kozi ni mpya lakini mpaka sasa tumeona matokeo mazuri kwa wanafunzi kwani wameweza kutengeneza vipodozi mbalimbali kama vile lotion, Lipstic, mafuta pamoja na viungo vya kupikia" amesema Dkt Moh'd.
Amesema kuwa, kupitia kozi hiyo wanafunzi huwagawa makundi ya kuanzia watu watano, hivyo wanaunda kampuni yao na wanafanya shughuli zao baadae huzisajili ili kwenda sokoni kwa ajili ya kununuliwa.
Mkuu wa Kitengo Cha Mahusiano na Masoko wa Chuo hicho, Khadija Mahumba, mesema kuwa, chuo hicho kimeongeza kozi mbili ikiwemo ya shahada ya awali ya sayansi ya maabara pamoja na shahada uzamili ya uendeshaji wa biashara na fedha ikiwa ni jitihada za chuo hicho kuhakikisha wanatoa elimu bora.
"Chuo kinatoa Shahada ya Ujasiriamali na Ubunifu ambayo imekuwa msaada mkubwa kwa wahitimu kuanzisha biashara na kujitegemea kwa kujiajiri hivyo amewashauri wazazi na walezi watembelee banda lao kujionea mazuri ya chuo" amesema
Post a Comment