UAR ILIVYOJIPANGA KUWASAIDIA WANAFUNZI KUSOMA NJE YA NCHI.
Na Francisco Peter, Dar es Salaam.
Taasisi Vyuo Vikuu Nchini (Universities Abroad Representative (UAR)) imeishauri Serikali ya Jamhuri ya Tanzania kuwa na utaratibu wa kutoa mikopo kwa wanafunzi wa naotaka kwenda kusoma nje y Nchi jambo ambalo litasaidia kuzalisha wataalam wenye uwezo mkubwa katika fani mbalimbali na kufikia malengo tarajiwa.
Akizungumza jijini Dar es Salaam katika maonesho ya Vyuo Vikuu yaliyoandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Tony Kabetha, amesema wanafunzi wengi wanapenda kusoma nje ya nchi ila wanakwama kutokana na changamoto ya fedha
"Naomba serikali kuwsaidia wazazi wa wanafunzi wanaosoma Vyuo vya nje ya nchi kwa kuwapa mikopo sawa na wanafunzi wa wanaosoma hapa nchini kuwapunguzia gharama," amesema Kabetha.
Kabetha amesema kwamba vijana wanaosoma vyuo vya nje wanafaida kwa Taifa kwani baada ya kumaliza masomo wanakuja kuwekeza nchini.
Amesema kuwa pia wanaongeza maarifa mapya kwa sababu nje wanakosoma kuna maendeleo ya kiteknolojia pamoja na kujifunza taaluma nyingine ambazo hazipatikani nchini.
Amesema kuwa taasisi hiyo imekuwa na utaratibu wa kuwasaidia vijana kupata nafasi katika nchi za ujerumani na hispania kwa ajili ya kuendeleza vipaji vyao.
"UAR ni taasisi ya kwanza kutoka hapa Tanzania kwa kuweza kusaidia vijana kusoma na kupata ajira nje ya nchi" amesema
Post a Comment