Ads

IRUWASA YAVUNJA RECORD HII

 


MAMLAKA ya Maji na Usafi wa Mazingira Iringa (IRUWASA) imevunja rekodi na kuongoza nchini kwa Kufunga Mita za Malipo ya Maji Kabla 6,752  ambazo zimekuwa suluhisho na kupunguza idadi ya wadaiwa sugu wa ankra za maji bila kulipa.


Akizungumza Jijini dodoma Mkurugenzi Mtendaji wa IRUWASA, David Pallangyo amesema, Mamlaka hiyo iliyoanza daraja C hadi sasa ipo daraja A na inajitegemea gharama za matengenezo na uendeshaji na sehemu ya uwekezaji, imefanikiwa katika eneo la TEHAMA kwa kufunga mita za malipo kabla kwa wateja hao.


Kutokana na kufunga mita za malipo kabla kwa viongozi wa serikali na taasisi mbalimbali, kumepunguza ongezeko la madeni ya watumiaji maji bila kulipa na kubaki deni la Sh bilioni mbili ambalo wadaiwa wengi ni watu wa kawaida.

Mamlaka hiyo pia imevuka lengo la Sera ya Maji ya 2002 na Ilani ya CCM ya kutoa huduma ya usambazaji maji kwa mji wa Iringa na maeneo ya pembezoni kwa kuunganisha wateja 40,459 sawa na asiimia 97 ya wakazi ambazo ni zaidi ya asilimia 95 zinazoelekezwa kwenye sera na Ilani.

Katika mpango wa muda mrefu, Serikali kupitia IRUWASA inakusudia kutekeleza mradi mkubwa wa uboreshaji huduma ya majisafi na majitaka katika manispaa ya Iringa, miji ya Kilolo pamoja na baadhi ya vijiji kando ya bomba la maji litakamopita.

Mradi huo unalenga kuanzisha  chanzo kipya katika mto Mtitu uliopo Wilaya ya Kilolo utaongeza upatianaji wa maji ya kutosha kwa miaka 20 ijayo na utaongeza utoaji wa majitaka zaidi ya asilimia 30 ya wakazi wa iringa kutoka asilimia 6.8 za sasa.

Pia Mradi huo utekelezwa kwa ushirikiano wa serikali kupitia mkopo wenye masharti nafuu kutoka serikali ya Korea wa US milioni 88.4 utaanza kutekelezwa Mei 2023 na ujenzi kuanza Aprili 2024 na utakamilika 2027.

Pallangyo amesema, mradi  utakapokamilika huduma za maji safi na salama kwa miji ya Iringa, Kilolo na Ilula zitafikia asiimia 100 kwa saa 24 kwa siku saba.

Jumla ya wananchi 456,010 watanufaika na huduma ya majisafi hadi mwaka 2045, huku wananchi 141,543 watanufaika na huduma ya uondoaji majitaka na Watanzania 6,455 watanufaika na kazi za mikataba na utachangia uchumi na ustawi wa jamii.

No comments