MSANII WA REGGAE KUTOKA NEW YORK KUTUA TANZANIA KUTAMBULISHA ALBUM YA 'SIDE OF THE TIME'
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES
SALAAM
Msanii wa Muziki wa Reggae
kutoka New York nchini Marekani Nat Sterling anatarajia kuja nchini Tanzania
kwa ajili kufanya ziara pamoja kutambulisha album yake mpya inayojulikana kwa
jina la 'Side of the time' kupitia
maonesho mbalimbali anayotarajia kufanya.
Katika album ya 'Side of the
time’ ina nyimbo 12 ambazo zimebeba
maudhui ya wapendanao yenye lengo ya kuelimisha jamii kuhusu maana ya siku ya
wapendanao kwani baadhi ya watu wengi duniani wanatafsiri siku hiyo tofauti.
Akizungumza na waandishi wa
habari leo jijini Dar es Salaam Mratibu wa ziara ya Msanii Nat Sterling,
Bw Dimateo Zion, amesema kuwa maandalizi
ya msanii huyo wa Reggae kutoka New York nchini Marekani kuja Tanzania
yanaendelea vizuri na anatarajia
kuwasili hivi karibuni.
Zion amesema kuwa lengo ya
ziara ni kutambulisha album yake kwa wadau wa nyimbo za reggae pamoja na
kuhakikisha wanashirikiana na wasanii wengine hapa nchini katika kuhakikisha
kwa namna moja au nyengine mziki wa Reggae unasonga mbele.
"Anatarajia kutambulisha
nyimbo 12 kupitia maonesho mbalimbali
atakayofanya, tunawaomba watanzania kutoa ushirikiano kwa msanii huyo wa
Kimataifa kutoka New York, Marekani" amesema Zion.
Katika album yake ya “Side of the
time” kuna nyimbo 12 ambazo ni Phantom, Viper, Moon light, Rasta shines, Nice,
You make me smile, Rock my world, Young Lady, Woman it's you, Your love, sign
of the time pamoja na Where is the love.
Post a Comment