MAKAMU WA RAIS AWASILI AZERBAIJAN KUSHIRIKI MKUTANO WA NAM
Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango amewasili katika mji wa Baku nchini Azerbaijan, ambapo anamwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa Nchi Zisizofungamana na Upande Wowote (Non – Aligned Movement - NAM) unaotarajiwa kufanyika Machi 02, 2023 nchini humo.
Katika mkutano huo, nchi wanachama wa NAM zitajadili namna ya kukabiliana na athari za UVIKO -19 pamoja na kuweka azimio la pamoja (NAM Vision on post-pandemic recovery).
Post a Comment