Ads

PMFUKO WA PSSF WAPATA FAIDA LUKUKI

 



Na. Wellu Mtaki, Dodoma

Kwa mwaka wa fedha ulioishia juni 2022,mfuko wa Psssf ulipata faida ya uwekezaji kiasi cha shilingi bilioni 581.72.

Hayo yameelezwa na CPA Hosea Kashimba Mkurugenzi mkuu Psssf wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma kuhusu maendeleo ya mfuko huo 

Amesema kutokana na uwekezaji huu,mfuko hupata faida ya uwekezaji ( return on investment) wastani wa asilimia 8 kwa mwaka,ambayo ni juu ya mfumuko wa bei na hivyo kufanya uwekezaji huu kuwa na tija.


Aidha mfuko wa psssf ni mmoja ya waendelezaji milki (real estate developers) wakubwa nchini,mfuko unamiliki majengo ya kupangisha katika miji mbalimbali ambayo hutumika kwa shughuli za kibiashara asilimia 72,ofisi na makazi asilimia 98.


Ameongeza kuwa wakati wa kuunganisha mifuko psssf ilirithi madeni ya serikali yaliyohakikiwa yenye thamani ya Tsh 731.40 bilioni,mpaka sasa kiasi cha Tsh 500 bilioni kimelipwa na serikali.


“ Nirudie kuishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kutambua deni la  michango kabla ya 1999 maarufu kama ( pre 99 liability) ambalo ni Tsh 4.60 trilioni kwa kutoa hafi fungani maalum yenye thamani ya Tsh 2.17 trilioni,haya yote yanaleta matumaini ya kuwa na mfuko wenye ustahimilivu na endelevu kwa ustawi wa wanachama” Amesema CPA Kashimba.


Aidha wakati wa kuunganisha mifuko,kiasi kilichokuwa kinalipwa kama pensheni kwa mwezi kwa wastaafu kilikuwa Tsh 34  bilioni,lakini mpaka kufikia sasa wastani wa kiasi cha Tsh 60 bilioni kinalipwa bila kukosa kwa wastaafu zaidi ya 150,000 kila ifikapo tarehe 25 kila mwezi.


“Mfuko umewekeza shilingi trilioni 4.5 katika hatifungani za serikali,pamoja na kuleta faida ya uwekezaji kwa mfuko kupitia riba na uwekezaji huu unauwezesha mfuko kutekeleza majukumu yake ya msingi" amesema kashimba.

Vilevile mfuko umewekeza zaidi ya shilingi bilioni 500 katika soko la hisa la DSM kupitia makampuni mbalimbali yaliyoorodhesha,uwekezaji huu mkubwa wa mfuko unasaidia kukuza soko la mitaji nchini na kuchochea uchumi na maendeleo ya mwananchi mmoja mmoja.


“Zaidi ya bilioni 400 zimewekezwa katika amana za muda (fixed deposit) katika benki mbalimbali hapa nchini,uwekezaji huu pia kwa mabenki kutoa mikopo mbalimbali kwa watanzania na hivyo kuharakisha azima ya serikali kukuza uchumi na kuinua” Amesema  Kashimba.

Kwa upande wake Msemaji mkuu wa serikali Ndg.Gerson Msigwa amewapongeza Psssf kwa taarifa za kukua kwa mfuko kwa asilimia 8 na kusema ni jambo zuri na inaonyesha jinsi gani mfuko umeweka mazingira mazuri kwa wanachama.


“Nimepata nafasi ya kutembelea ofisi za Psssf na nimeridhishwa na namna ambavyo mfuko unafanya kazi zake na kuimarisha huduma kwa wafanyakazi,pia wafanyakazi ni muhimu kufuatilia michango yao inapowasilishwa na kujiridhisha” Amesema Msigwa.



No comments