Ads

RC DODOMA AMETAKA UJENZI UKAMILIKE KWA HARAKA.



 Na. Wellu Mtaki, Dodoma

Mkuu wa mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amewataka wakuu  wa shule wote waliokabidhia fedha za ujenzi wa madalasa katika mkoa wa Dodoma kukamilisha miradi hiyo Ifikapo tarehe 20 november mwaka huu.

Hayo ameyasema jijini dodoma wakati wa ziara ya kutembelea baadhi ya shule kuona muendelezo wa hatua zilizofikiwa katika shule hizo huku akifafanua kuwa Rais Samia Suluhu Hassan alitoa fedha kwa ajiri ya kuwawezesha watoto wanaokwenda kidato cha kwanza mwaka 2023 wasikose darasa ya kusomea .

Amesema kuwa mkoa wa Dodoma ulipata shilling Billion 6 na milioni 780 kwa ajiri ya ujenzi wa madalasa 339 ambapo fedha hizo zimegawanyika katika shule mbalimbali mkoani hapo.

Pia  Senyamule amewataka walimu wa shule ya sekondari zuzu kuongeza juhudi za ufundishaji katika shule hiyo ili kuongeza ufahuru kwa wanafunzi.

KWa upande wake Mkuu wa shule ya sekondari Zuzu  Hezron Lupondo  amesema kuwa shule ya sekondari Zuzu ilipata shilling million ishirini KWa ajili ya ujenzi wa chumba kimoja cha darasa na ofisi huku akimuhakikishia Mkuu wa mkoa wa Dodoma watafanya kazi usiku KWa mchana kukamilisha ujenzi huo pamoja na kuongeza ufahuru katika shule hiyo.

Naye Mkuu wa shule ya sekondari Mnadani   Claudian James Kabuyombo amesema kuwa anaishukuru Serikali ya Awamu ya sita KWa kuendelea Kuimalisha sekta ya elimu Tanzania.

No comments