Ads

MAKADA WA CCM WAJITOSA KUSAIDIA UJENZI NYUMBA YA KATIBU MKUU CCM MKOA WA DAR.

Diwani wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Viti Maalum, Kata ya Upanga Mashariki Jijini Dar es Salaam Bi. Beatrice Edward kwa kushirikiana na Mjumbe wa Halmashauri Kuu Manispaa ya Kinondoni Bi. Asha Mohammed  wamekabidhi mifuko 10 ya saruji kwa uongozi wa Chama cha CCM  Mkoa wa Dar es Salaam kwa ajili ya kukamilisha ujenzi ya nyumba ya Katibu Mkuu wa Chama hicho.

Akikabidhiwa mifuko ya saruji Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam, Adam Ngalawa,  ameshukuru kwa kupokea mifuko ya saruji  kwani inaenda kumaliza wa ujenzi wa nyumba.

"Nimefurahishwa na wanachama wetu Mkoa wa Dar es Salaam, kuendelea kujitolea vitu mbalimbali kwa ajili ya kukamilisha ujenzi "amesema Ngalawa.

Ngalawa amesema kuwa ujenzi wa nyumba tayari umefikia hatua ya umaliziaji, uku akibainisha ujenzi wa nyumba ulianza  mwezi juni 2022 na unatarajiwa kukamilika mwezi Disemba, 2022.

Amesema kuwa mpaka sasa tayari zimetumika Sh.milioni 90 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa nyumba hiyo.

Wanachama wa Chama cha CCM Mkoa wa Dar es Salaam walianza kuchangia ujenzi Oktoba 22, 2022 wakati wa uwekaji jiwe la msingi uliofanywa na Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Daniel Chongolo.

No comments