SERIKALI YASITISHA SHUGHULI ZA KIBINADAMU KATIKA MTO RUAHA MKUU .


SERIKALI imewataka
wananchi wote wanaofanya shughuli za kibinadamu katika vyanzo vya Maji
wasitishe shughuli mara moja kutokana na athari zinazoendelea katika Mto Ruaha
Mkuu (GREAT RUAHA) zinazosababishwa na kilimo,ukataji
wa miti hovyo pamoja na ufugaji wa mifugo unaosababisha mto huo kukauka.
Akizungumza kwenye mkutano
wa mawaziri nane uliofanyika Makao Makuu ya Hifadhi ya Ruaha iliyopo Msembe
mkoani Iringa,Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano
Dk.Seleman Jafo kwa niaba ya waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Kassim Majaliwa alisema kuwa kukauka Mto Ruaha Mkuu (GREAT RUAHA) umeathiri shughuli za kiuchumi ikiwemo mgao wa
umeme pamoja kutokuwa na maji ya matumizi ya nyumbani katika mkoa wa Dar es
Salaam
Dk.Jafo ameagiza bodi za
bonde za maji na Baraza la Udhibiti na Usimamizi wa Mazingira kusimamia vyanzo
vya maji kwa wale waliochepusha na wale wanaotumia maji kwa mujibu wa vibali
kuangalia suala hilo.
Amesema kuwa suala la
Ruaha tangu 1994 maji yanaacha kutiririka mwezi wa tano hiyo ni kutokana na
shughuli za kibidamu kuendelea kwenye vyanzo vya maji.
Dk.Jafo alisema kwa
kipindi hiki wanyama wakiwemo viboko,Mamba na aina mbalimbali za samaki wapo
katika hali mbaya hivyo tuombe mvua zinyeshe kwa kipindi kifupi ili kuwaokoa
wanyama hao waendelee kuishi vinginevyo watakufa.
“Mto Ruaha umekauka kabisa
tulikuwa tukipita na helikopta kule juu mto umekauka kabisa mto huu hauna maji
kabisa yanayotiririka hata ukienda Ihefu hali ni mbaya sana inaenda sambamba na
kuathiri sekta nyingine
mfano mzuri sekta ya nishati mimi naaminiu kiwango cha umeme kinachozalishwa na maji leo hii inawezekana ukienda mtera naamini kiwango cha umeme kinachozalishwa katika mabwawa haya hali imekuwa ni mbaya sana” Dk.Jafo
alisema kuwa kupitia sheria ya
maji ya mwaka 2022 Seleman Jafo aliwataka wakulima kuacha mara moja kulima na
kuchepusha maji ya mto Ruaha kinyume na taratibu huku akiwataka kuondoka haraka
na kuiagiza mamlaka ya bonde kusimamia sheria hiyo
Kwa upande wake Waziri wa
Utalii Balozi Dkt.Pindi Chana alisema kuwa wananchi wanatakiwa kushikamana ili
kulinda na kutunza maliasili zilizopo pamoja na vyanzo vya maji.
“Wote tulioingia hapa
tumeshuhudia kwamba Mto Ruaha Mkuu (GREAT RUAHA)
umeanza
kukauka nitumie nafasi hii kuutangazia umma na watanzania wenzangu jukumu ni kutunza
na kuendeleza maliasili kwa hiyo nawaombeni sana tushirikiane na kuendeleza
hifadhi zetu na kuna vyanzo vya maji mengi sana vitasaidia idadi yetu kwa sensa
ya mwaka huu maji haya pia yanasaidia hifadhi zetu”
Naye Kamishina wa
Uhifadhi wa Shirika la Taifa la Uhifadhi (TANAPA) William Mwakilema alisema
ukame wa Mto Ruaha ni hatari kwa wanyama na hii ni kutokana bonde la
Usangu/Ihefu kuendelea kwa shughuli za kilimo za kuzuia maji kwenye mto Ruaha.
Mwakilema amesema
jitihada mbalimbali zinafanyika za kuweza Mto Ruaha kuwa na maji kwa vipindi
vyote kutokana na mto huo kuwa na tegemeo kwa Taifa.
“Kipindi hiki ambacho mto
umekauka ni kipindi kigumu kwa sababu wanyama wanataabika kupata maji wanyama
kupata chakula maeneo ya kupumzika siyo mazuri lakini pia tunaona sisi ambao ni
wasimamizi tunawakati mgumu pia kuangalia cha kufanya hali ya mto ruaha sio
nzuri na jitihada mbalimbali zinapaswa kufanywa ili kuhakikisha huu mtoto unatirirsha
maji vinginevyo uhai wa mto huu utakuwa mashakani “alisema Mwakilema
Kabla ya mkutano huo
umechukua masaa matatu ya viongozi kujadiliana kutokana na hali waliokuta
katika mto Ruaha ukiwa umekauka.
Post a Comment