WALIOKWENDA ISRAEL KULIOMBEA TAIFA LA TANZANIA WASIMULIA UKUU WA MUNGU.
Baadhi ya waumini wa dini ya kikristo kutoka madhehebu mbalimbali kutoka nchini Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja nchini Israel kwa ajili kujifunza biblia kwa njia ya vitendo pamoja na kufanya maombi (kuliombe Taifa la Tanzania).
Baadhi ya waumini wa dini ya kikristo kutoka madhehebu mbalimbali kutoka nchini Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja nchini Israel walipokwenda kwa ajili ya kufanya maombi katika nchi hiyo Takatifu.
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM.
Waumini ya dini ya kikristo zaidi ya 80 kutoka madhehebu mbalimbali wamewasili Tanzania kutoka nchini Israel walipokwenda katika safari ya kiimani kwa ajili ya kufanya maombi katika nchi hiyo Takatifu.
Safari hiyo ya kiimani imeratibiwa na Kanisa la KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani Kwa kushirikiana na Kampuni ya Yerusalemu Hold Land Pilgrim ambayo ina lengo la kufanya maombi kwa ajili ya kuliombe Taifa pamoja na kuendelea kujifunza neno la Mungu kwa njia ya matendo.
Akizungumza leo tarehe Novemba 16, 2022 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam baada ya kuwasili kutoka nchini Israel, Mchungaji Kiongozi wa KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani Charles Mzinga, amesema kuwa washiriki 86 wamefanikiwa kwenda katika safari hiyo ya kiimani na maombi.
Mchungaji Mziga amesema kuwa Mungu wetu ni mpya kila siku tumekuwa tukimuomba katika kufanikisha mahitaji yetu mbalimbali.
Amehimiza wakristo kuhifadhi na kutunza fedha kidogo kidogo kwa ajili ya kutembelea Israel na kushuhudia maeneo ambayo Bwana Yesu alizaliwa na kufanya kazi.
Amesema hayo baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere, akitokea ziara ya kimaombi nchini Israel, iliyoandaliwa na KKKT Azania Front kwa kushirikiana na kampuni ya Jerusalem Holly Land Pilgrim.
Post a Comment