Ads

BODI YA KOROSHO YADHAMIRIA KUONGEZA UZALISHA WA KOROSHO.

 Na. Wellu Mtaki, Dodoma.

Bodi ya korosho Tanzania chini ya wizara ya kilimo na serikali imepanga kuzalisha korosho tan laki 7 ifikapo mwaka 2025 - 2026 pamoja na kuanzisha mashamba makubwa ya pamoja.

Hayo yamesemwa na kaimu mkurugezi wa bodi ya korosho nchini  francis Alfred wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini dodoma kuhusu utekelezaji wa shughuri mbalimbali za taasisi hiyo pamoja na muelekeo wa utekelezaji wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2022/ 2023.

Aidha Alfred amesema kuwa pamoja na lengo hilo la uzalishaji wa korosho nchini kutoka wastani wa chini ya 10/% ya uzalishaji hadi 60% ifikapo mwaka 2025.

Pia amesema kuwa bodi ya korosho nchini itashirikiana na bodi ya usimamizi wa stakabadhi ya ghala la tume ya maendeleo ya Ushiriki zimeandaa na kutoa muongozo wa masoko na mauzo ya korosho kwa msimu 2022/2023.

Pamoja na hayo ameeleza kuwa bodi ya korosho imejipanga kuongeza Maeneo ya uzalishaji wa korosho nchini kutoka mikoa mitano iliiyokuwa ikizalishwa hapo awali hadi kufikia mikoa Zaidi ya 17 kwa sasa.


No comments