MIPANGO CHAONGEZA KOZI MPYA
Na. Wellu Mtaki , Dodoma.
Katika kuhakikisha kunakuwepo na wigo mpana wa ajira Chuo cha mipango ya maendeleo vijijini chaongeza cha Jijini Dodoma kimeanzisha kozi mpya za tehama, upimaji ardhi pamoja na uhasibu na fedha.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Baraza la uongozi wa chuo cha mipango ya maendeleo vijijini prof Martha Qorra wakati akizungumza na wahandishi wa habari jijini dodoma katika ufunguzi wa kongamano la kufanya mapitio ya baadhi ya mitaala ya zamani na mitaala mipya ambayo inaanzishwa chuoni hapo.
Naye mkuu wa chuo hicho prof Huzen Mayaya ,amesema kozi zinazotolewa na chuo hicho cha serikali ni bora na zinakwenda kuwasaidia wahitimu wengi kupata zana ya kujiajiri wenyewe.
Kwa upande wake makamu mkuu wa chuo cha mipango ya maendeleo vijijini anayeshughurika na taaluma , utafiti na ushauri prof provident Dimoso amesema chuo kinajikita katika utoaji wa elimu Kwa vitendo ili kusaidia wimbi la wahitimu kujiamini na kuelewa zaidi hata waendapo mitaani waweze kujiajiri na kuwa na sifa za kuajiriwa.
Chuo cha mipango ya maendeleo vijijini ni chuo kilichoanzishwa KWa lengo la kusaidia vijana baada ya kufanyika utafiti kugundulika ipo haja ya vijana kuwa na mipango ambao hitawaaaidia katika maisha yao.
Post a Comment