Ads

WENYEVITI WA MITAA KIGAMBONI ;TUNAMATARAJIO MAKUBWA BAADA YA SENSA .

 



Na John Luhende 

Mwamba wa habari

Wenyeviti wa Serikali za mitaa  Manispaa ya Kigamboni Mkoani Dar es salaam, wamesema kuwa baada ya kukamilika kwa zoezi la sensa ya Watu na makazi wanaimani kutafanyika mabadilko makubwa ya kiuchumi katika maeneo yao.

Wenyeviti hao wametoa kauli hiyo wakati wakizungumza na Mwamba wa habari blog kwa nyakati tofauti.

Mweneviti wa wenyeviti ambaye pia ni Mwenyekiti wa mtaa wa Shirikisho  kata ya Somangila  Ndugu ,Hassan Babu Said, amepongeza namna zoezi la Sensa lilivyo fanyika wilani humo akisema kuwa kulikuwa na ushirikiano mkubwa kutoka kwa viongozi wa Serikali.

''Napenda kwanza kabisa nimpongeze Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ,kwa namna ambavyo amefanikisha zoezi hili kwa kupanga safu ya viongozi wachapa kazi hususani katika wilaya yetu ya Kigamboni, Mkuu wetu wa wilaya amekuwa akihamasisha kwa hali zote na alitutembelea katika mitaa yetu yote akafanya mikutano na wananchi wetu hivyo walikuwa na ulewa mkubwa kuhusu sensa ''Alisema 

Aidha amesema, katika mtaa huo wananchi ambao walipitwa na makalani waliitikia wito uliotolewa na kamisaa wa Sensa walifika katika ofisi za mtaa na walihesabiwa.

Aidha amesema kuwa anaimani kuwa Serikali itakuwa imepata idadi sahihi ya watu na makazi kwa kuwa zoezi lilifanyika kwa uwazi na kila mwananchi alishiriki kwa kutoa ushirikiano kwa  makalani wa Sensa .

''Naamini kupitia Sensa hii Serikali imesha fahamu mahali ambapo hakuna  miundombinu na huduma za kijamii na kwamba watauletea mfano hapa katika mtaa wetu hatuana shule ya Msingi  , Zahanati na hatuna maji'' Alisema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa  mtaa wa Majengo kata ya Vijibweni Thomasi Manyama Pamoja na kupongeza namna ambavyo zoezi la Sensa limeendeshwa, amesema wanayo matarajio makubwa kuona changamoto zilizo kuwa zinaikabili kata  na mtaa wake zita kuwa zimepatiwa ufumbuzi pindi bajeti itakapo pitishwa .

''Kata yetu  ya Vijibweni ina watu wengi tunamatumaini kwamba baada ya zoezi hili kwa kuwa tunahitaji shule ya msingi Bopwe na shule ya Selitakuwa limepata suluhisho.

Naye Mwenyekiti wa Mtaa wa Vijibweni  Mohamed  Athumani Zigo, ameshukuru viongozi wa serikali kuu kwa namna walivyowahamasisha wenyeviti hao katika zoezi hilo jambo ambalo lilirahisisha utoaji wa taarifa kwa wananchi.

Amesema kata ya Vijibweni imekuwa na ongezeko la watu kutokana na kichocheo cha Daraja Nyerere  hivyo Sensa hii itatoa majibu sahihi na kwamba mgawanyo wa fursa za maendeleo na ujenzi wa huduma za kijamii pamoja na  Miundo mbinu zita fanywa kutokana na idadi halisi ya wakaazi.

''Nikiri kuwa tangu kukamilika kwa Daraja la Nyerere watu wengi wamehamia mtaa wa Vijibweni na kata hii kwa ujumla na kumekuwa na changamoto za kiusalama lakini nashukuru Mungu kwa kushirikiana na viongozi wenzangu kumekuwa na mikakati ya ulinzi shirikishi na hali ya usalama hapa imetulia ''Alisema 

Katika siku za hivi karibuni katika kata ya vijibweni kumeripotiwa taarifa za makudi ya uhalifu ambapo siku chache zilizopita vijana kadhaa walikamatwa katika tukio la wizi wa kunja nyumba.

No comments