Ads

RC MGUMBA WANAOWEKA FEDHA KWENYE MAGODORO WAMEPUNGUA

 




Na Oscar Assenga,TANGA


SERIKALI mkoani Tanga imesema

kwamba kusogezwa karibu kwa huduma za kibenki kumesaidia kupunguza

wananchi waliokuwa wakihifadhi fedha zao kwenye magodoro jambo ambalo

ilikuwa ni athari kubwa ikitokea wizi inakuwa rahisi kuweza kuibiwa au

kupotea lakini pia zimekuwa salama na hivyo kuepukana na matumizi

yasiyokuwa ya lazima.


Hayo yalisemwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga

Omari Mgumba wakati akifungua tawi jipya la Benki ya NMB Ngamiani

lililopo barabara ya 20 Jijini hapa katika halfa iliyokwenda sambamba na

utoaji wa mabati 250 kwa shule ya msingi Masiwani.


Alisema uwepo wa tawi hilo utawawezesha wananchi kupata sehemu ambayo yataweza kuhifadhi fedha zao walizozitolea jasho na kuondoa changamoto ya

uhifadhi kwenye vyungu vya maji au kulalia kwenye magodoro ambapo

ikitokea moto au wizi kuiba kwake inakuwa ni rahisi lakini pia fedha

zina vishawishi ukiziweka ndani matumizi yake yanakiwa ni makubwa sana.


Mkuu huyo wa mkoa alisema lakini ikiziweka benki unaweza kuokoa matumizi

yasiyokuwa yalazima na unaweza kutumia hapo baadae kwenye matumizi

muhimu katika mahitaji na maisha yenu.


Alisema Serikali imeweka mazingira mazuri kuhakikisha jamii ya kitanzania inapata huduma Bora sa kibenki na nafuu huku akiishukuru benki hiyo ambayo imekuwa ikiunga mkono juhudi za Serikali na hivi karibuni mlitenga zaidi ya

Bilioni 200 ya mikopo kwenye sekta ya kilimo kwa riba ya asilimia 9.


“Niwapongeze Benki ya NMB kwa kuendelea kubuni huduma mpya kwa kufungua matawi mapya na zaidi ya hapo kuwajali na kuwathamini wateja bila kujali kipato pia serikali inatambua juhudi zenu za kuwawezesha wananchi kupitia mikopo ya wafanyakazi,wakulima na wafanyabiashara wakubwa na wadogo” Alisema Mkuu huyo wa Mkoa


Alisema dunia kwa sasa inakwenda kasi

hususani kwa upande wa teknolojia ambazo zimerahisisha huduma za kibenki

kutokutegemea matawi rasmi ingawa haiondoi ukweli kwamba kufungua

matawi mapya ni kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi ambao hauwezi

kupata nje ya tawi la benki.


Mkuu huyo wa mkoa alisema pamoja

na mafanikio yaliyoyapata katika kubuni huduma bora na nafuu na za

haraka ikiwemo huduma mpya ya Teleza Kidigitali ambayo kwa mara ya

kwanza benki inatoa mikopo midogo midogo bila kufika kwenye tawi la

benki bila kuwa na dhamana unakopa mwenyewe kupitia simu ya mkononi.


Alisema

mikopo hiyo itaondoa adha kwa mama mntilie,babalishe na watu wengine

wenye biashara ndogondogo ambao mitaji yao haizidi laki tano hiyo

inafaida kubwa ya matumizi ya teknolojia kwani wananchi wengi hususani

wafanyabiashara wadogo wadogo huduma hiyo itawanufaisha sana.


Aidha

alisema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu

imaweka mikakati mizuri ya kupunguza umaskini kwa wananchi wake hivyo

nitoe changamoto kwa ajili ya kuwasaidia na kukuza ajira kwa wananchi

kuendelea kutoa mikopo kwa wakazi wa vitongoji vyote vya mkoa wa Tanga

mijini na vijijini.


Awali akizungumza wakati wa halfa

hiyo,Afisa Mkuu na Wateja wakubwa na Serikali wa Benki ya NMB Alfred

Shayo alisema kwamba benki hiyo imekuwa ikiendeshwa kwa waledi na

ufanisi na ndio maana wameweza kufikia hatua kubwa ya kimaendeleo hapa

nchini


Alisema tokea Benki hiyo ilipoanzishwa mwaka 1997

imepiga hatua kubwa kwani awali ilikuwa na matawi 97 lakini sasa matawi

yamefikia 227 na uzinduzi wa tawi hilo unaongezeka na kufikia 228 ni

hatua kubwa imefanya ili kuweza kuwafikia wateja wake kwa karibu zaidi

ambapo usogezaji karibu huduma kwa wananchi hatujaaachwa nyuma

kidigitali.


” Benki ilipoanzishwa ilikuwa haina wakala wala

ATM lakini kwa sasa ina na atm 762 na mawakala zaidi ya 15000 hii

inaonyesha namna mnavyoishi ndoto zenu Benki ua NMB karibu yako na

kujipanua kwenye mtandao na tunafanya kazi karibu na Serikali pamoja na

wateja wetu kuhakikisha tunaboresha huduma na kutoa masuluhisho kwa

wateja wetu”Alisema.


Alisema kwa mwaka jana wametoa trilioni

4.3 za mikopo kwa wateja wadogo wadogo kwa kilimo, biashara ndogondogo

na wateja binafsi hiyo imetokana na ushirikiano mzuri walionayo kati yao

na Serikali na wateja wao


“Kwa Tanga Benki wetu ya NMB ina

matawi 10 kanda ya kaskazini tuna matawi 40 hii inaonyesha namna gani

tupo karibu na serikali huku wananchi wanapata masuluhisho ya

kuwasaidia kuendeleza shughuli za kuweza kujikwamua kiuchumi”Alisema


Alisema

kwa upande wa Kilimo kama walivyosikia serikali ilitoa trilioni 1 kwa

ajili ya kukopesha sekta ya kilimo kwa riba ambayo ni ya chini ya

asilimia 10 huku akieleza kwamba hawakwenda kuchukua hela benki kuu

Tanzania (BOT) hivyo walitenga fedha zao Bilioni 100 kwa ajili ya

kukopesha kwa asilimia 10 ilipoisha na wakatenga nyengine bilioni 100

ambayo wanapokesha wakulima wadogo wadogo kwa riba ya asilimia 9.


Naye

kwa upande wake Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini Prosper kwa

niaba ya Benki alisema kwamba wamefarijika sana kuona mwitikio kutoka

kwa wananchi waliojumuika katika shughuli hiyo muhimu ya uzinduzi wa

tawi hilo ambapo ni utekelezaji wa azma yao ya kusogeza huduma karibu na

wana chi.


Naye kwa upande wake Meneja wa Uchumi na Takwimu

Benki kuu ya Tanzania (BOT) tawi la Arusha Ernest Ndunguru alisema

baadhi ya Benki zimekuwa na tabia ya kutokuweka fedha kwenye ATM mashine

hususani nyakati za sikukuu na wikiendi jambo ambalo zimekuwa kero kwa

wananchi wengi.


“Mimi ni moja ya wateja wa Benki hapa nchini

lakini changamoto kubwa ambazo umekuwa tukikutana nazo ni kukosekana

kwa fedha kwenye ATM Mashine hususani nyakati za sikukuu na wikiendi

hili tatizo tunaomba lishughulikiwe “Alisema

No comments