Ads

CHUO KIKUU CHA RUCU KILIVYOBORESHA UTENDAJI WAO.

 

Mkurugenzi wa Kozi za Shahada na zisizokua za Shahada wa Chuo Kikuu cha Katoliki Ruaha( RUCU) Dkt Wille Migodela (wa kwanza kutoka kushoto) akitoa maelekezo kwa baadhi ya Wanafunzi waliotembelea banda la gov ya Tume ya Vyuo Vikuu Nchini (TCU) yanafofanyika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.

Chuo Kikuu cha Arusha kinachomilikiwa na Kanisa la Wadventist Wasabato  kimesema kwamba kinaendelea kutoa Elimu pamoja kuwajenga wahitimu Kiakiri  na kiroho ili kuwafanya wafikie ndoto zao nakuleta mchango mzuri wa Maendeleo 

Na Francisco Peter

Chuo Kikuu cha Katoliki Ruaha (RUCU) katika kuhakikisha kinakabiliana na changamoto zinazoikabili Jamii kimejikita kutoa Elimu kwa wanafunzi Kwa kufanya ubunifu wa tafiti mbalimbali Kwa ajili ya kukabiliana na changamoto za kimazingira Kama vile Mbu wanaoambukiza Ugonjwa wa Malaria.

Magonjwa Mengine ni magonjwa ya ngozi( Fangasi) na Kikohozi,ambapo wanafunzi wanafanya tafiti kupitia mimea ya asili nakutengeneza dawa ambazo zinasaidia kukabiliana na magonjwa hayo.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Kozi za Shahada na zisizo za Shahada wa Chuo hicho Dakt Wille Migodela wakati akizungumza na Waandishi wa habari kwenye maonyesho ya 17 ya Elimu y juu Sayansi na Teknolojia yaliyoandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu Nchini ( TCU).

Aidha amesema kwamba chuo hicho kinatoa program za Kozi mbalimbali lakini Elimu ya utafiti wa Ubunifu imekua ikipewa kipaumbele ili kumsaidia mwanafunzi anaehitimu kuondokana na zana ya kutemea kuajiliwa na badala yake aweze kujiajiliwenyewe.

Hata hivyo amendelea kusema kwamba Wanafunzi hao wamefanikiwa kubuni kifaa kinachopima uzito wa mizigo inayobebwa na magari ambapo kifaa hicho kinafungwa kwenye gari na gari hiyo haitapita kwenye mzani Kwa ajili ya kupimwa, badala yake kifaa hicho kitaonyesha ukomo wa  uzito kamili unaohotajika kubebwa na gari hilo.

"Magari yanatumia muda mrefu kukaa kwenye foleni ya mzani kupima uzito wa mzigo,sisi kama RUCU tumekuja na suluhisho la kubuni kifaa Cha kisayansi kitakachoonyesha ukomo wa uzito wa mzigo unaotakiwa kupakiwa" amesema Dkt Migodela

Amesema kwamba Kwa mwaka huu wa masomo 2022/ 2023 wanatarajia kudahili  wanafunzi wapatao 1400 ambapo wanafunzi wa Cheti na Diploma ni 700 na wengine 700 ni Shahada(Digree),ambapo amesisitiza kwamba mazingira ya kujisomea Kwa wanafunzi ni mazuri.

No comments