Ads

Chuo Kikuu cha Arusha kinachomilikiwa na Kanisa la Wadventist Wasabato wafanya makubwa.

 Chuo Kikuu cha Arusha kinachomilikiwa na Kanisa la Wadventist Wasabato kimesema  kinaendelea kutoa Elimu pamoja kuwajenga wahitimu Kiakiri  na kiroho ili kuwafanya wafikie ndoto zao nakuleta mchango mzuri wa Maendeleo Kwa Taifa.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kitengo Cha Masoko wa Chuo hicho Elisha Lomay wakati akizungumza na Waandishi wa habari kwenye maonesho ya 17 ya Elimu ya Juu,Sayansi na Teknolojia yaliyoandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu Nchini( TCU) yanayofanyika mnazi Mmoja Jijini Dar es salaam.

Aidha Lomay amesema kwamba chuo hicho kinatumia falsafa ya kumjenga mwamanafunzi akue katika maadili ya kiroho ,Kimwili, pamoja na kitaaluma ambapo wahitimu wengi wamekuwa wakifanikiwa kufanya kazi Kwa weledi mkubwa.

Amesema kwa chuo hicho ambacho kinapatikana pembezoni mwa Wilaya ya Meru Mkoani Arusha kimekua kikidahili wanafunzi bila gharama yoyote kupitia mtandaoni(Application fee bure) ,nakwamba baada ya wanafunzi kujiunga na chuo hicho wanalipia ada ambazo Wanaweza kuzimudu.

"Chuo chetu kinatoa ufadhili( Scholarship ) Kwa wanafunzi wanaotaka kusoma nje ya nchi Kwa kushirikiana na wasabato wenzetu wanaoishi nje ya nchi ikiwemo Marekani,hivyo tunawakaribisha wazazi na walezi kuwaleta watoto wao kujiunga na chuo chetu kwani kina mazingira rafiki yakujisomea na gharama za ada na hosteli ni nafuu" amesema Lomay.

Aidha amesema kwamba program wanazofundisha chuoni hapo ni pamoja na  Shahada ya Utawala wa Biashara na Uhasibu,Shahada ya Sanaa ya Ualimu,Shahada ya Sanaa ya Masomo ya Dini,pamoja Cheti na Astashahada ya Elimu ya Dini,

No comments