Ads

CHUO KIKUU CHA TAIFA CHA ZANZIBAR KILIVYOJIPANGA KUBORESHA SEKTA YA ELIMU.


Baadhi ya watu wakitembelea banda la Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar katika maonesho ya  ya 17 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia kupitia Tume ya Vyuo Vikuu ( TCU) anayofanyika jijini Dar es Salaam.

Na Francisco Peter.

Chuo Kikuu cha Taifa Cha Zanzibar (SUZA) kimejipanga kuendelea kutoa shirikiano katika sekta ya elimu nchini kwa kuanzisha kozi mpya ya  Shahada ya Uzamivu kwenye Sayansi ya Teknolojia ya Habari (IT) katika mwaka wa masomo 2022/ 2023.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonesho ya 17 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia kupitia Tume ya Vyuo Vikuu ( TCU) Mkuu wa Kitengo Cha Uhusiano na Masoko wa SUZA Bi. Khadija Sadiq Mahumba, amesema kwamba chuo hicho kinatarajia kudahili wanafunzi 2,000 kwa programu mbalimbali ikiwemo za Elimu, Afya, Kilimo kwa ngazi ya Cheti, Astashahada( Diploma) Shahada (Degree), Shahada ya Uzamili na Uzamivu.

Amesema kuwa kwa mwaka huu wa masomo chuo hicho pia kinatarajia kutoa programu ya Shahada ya Uzamivu( Phd) ya Lugha ya kiswahili ,na kwamba amewaomba wanafunzi wanaotaka kujiunga na SUZA wachangamkie fursa hizo.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Uhusiano na Masoko SUZA amesema kwamba Chuo hicho kinatoa programu za Kozi za Utalii ambapo wanafunzi watakaosoma kozi hizo watapata fursa ya kusoma lugha mbalimbali za kigeni ikiwemo lugha ya Kireno,Kichina ,Kifaransa,Kijerumani,na kwamba chuo hicho pia kinatarajia kuanza kufundisha Programu ya lugha ya Kikorea.

Hata hivyo amebainisha kuwa wakati wa udahili wa dirisha la pili wanatarajia kudahili wanafunzi kwa program mpya za Shahada ya Uzamili ya Benki na Fedha( MSc Benking & Finance) pamoja na Shahada ya Uzamili ya  Utawala wa Fedha na Biashara ( MBA-Finance).

"Ningependa kuwaomba wazazi wawalete wanafunzi  kwenye banda letu hapa Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam wajionee kozi tunazofundisha ili wafanye maamuzi sahihi yakujiunga na chuo chetu chenye fursa ya kupata ajira nje na ndani ya nchi" amesema Khadija

 

No comments