MKURUGENZI COSTECH AZINDUA PROGRAMU YA PesaTech Accelerator.
Mkurugenzi
Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dkt. Amos Nungu
amezindua programu ya PesaTech Accelerator inayolenga kukuza mawazo ya kibunifu
kwa ajili ya mifumo ya Sekta ya Fedha nchini.
Halfa
ya uzinduzi huo imefanyika katika ukumbi wa ZO Space (mkabala na Millenium
Tower), jijini Dar es Salaam, ambapo Dkt. Nungu amesema kuwa "Serikali
kupitia COSTECH, tunajivunia kwa kuwa
tumeendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wabunifu hapa nchini, program
tuliyoizindua hii leo itawasaidia wabunifu nchini kuongeza maarifa, kujenga
mtandao, na kupata fedha kwa ajili ya kuendeleza bunifu zao"
"Jana
tarehe 4 Mei 2022, Mh. Rais katika mahojiano na ndg. Mhando wa Azam TV, alisema
jinsi ubunifu unavyowezesha vijana kujiajili na kutoa ajira kwa wenzao ambapo
aliitaja Magilla na Maxcom wakiwa ni mfano wa wanufaika wa kumbi za bunifu
kupitia COSTECH" amesema Dkt. Nungu.
Dkt.
Nungu amewataka wabunifu wa mifumo ya kifedha nchini kujitokeza kwa wingi
katika kushiriki katika hiyo program ya PesaTech Accelerator ili wapate fursa
ya kujengwa na kuunganishwa na wafadhili mbalimbali – kujenga kampuni changa
nyingine mfano wa Nala inayoongozwa na Benjamini Fernandes ambaye amepata
uwekezaji wa Fedha za kimarekani milioni kumi.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Sahara Ventures, Jumanne Mtambalike alieleza kuwa “Tutafanya
kazi hii kwa karibu kabisa na COSTECH, tuko hapa na Mkurugenzi Mkuu Dkt. Nungu
vileivile tunashirikiana na wadau muhimu kama UNCDF lengo likiwa ni kutambua vijana wenye mawazo
ya kibunifu kwa kuwapatia msaada wa
kifedha, kiufundi, nyenzo pamoja na msaada wa kibiashara ikiwemo kupatiwa
mitaji ili mawazo yao yaingie sokoni na kuleta tija katika jamii” alisema
Bi.
Anneth Kasebele amesema kuwa Shirika la Kimataifa la Mitaji - UNCDF kwa
kushirikiana na Serikali na makampuni
binafsi wataendelea kusaidia miradi ambayo imejikita kwenye mifumo ya kifedha na bunifu za mageuzi ya kidigitali
kupitia sekta za kifedha. Aliongeza kuwa dira yao ni kusaidia kuchochea
jitihada zilizopo na kupanua wigo wa huduma ndani na nje ya nchi.
Mkurugenzi
wa Uendelezaji Masoko na Utafiti toka Mamlaka ya Masoko, Mitaji na Dhamana
(CMSA), Bw. Alfred Mkombo amesema kupitia uzinduzi huo wabunifu katika sekta ya
fedha nchini wataweza kusaidiwa kwa kuendeleza mawazo yao eneo la fedha, masoko
na mitaji na kwa kuendelea kutoa miongozo itakayosaidia kutoa mawazo mapya yatakayoleta maendeleo hapa nchini.
Uzinduzi
huo ulihudhuriwa na wadau wa ubunifu
nchini wawezeshaji kwa maana ya UNCDF na Ubalozi wa Swedish; washirika wa mradi: Sahara Ventures,
Enea Advisors, Hindsight Ventures ;
pamoja na wadau wa Sekta za Kifedha zikiwemo Taasisi ya Flutterwave, CRDB, Mwalimu bank na Wabunifu wa Tunzaa, Tausi, na Bizzyn.
Post a Comment