Ads

TARURA WAONDOLEWA KUKUSANYA USHURU WA MAEGESHO.

 Waziri  wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Innocent Bashungwa.

Na, Vestina Mlandali, Dar es Salaam.

Waziri  wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Innocent Bashungwa ameagiza kazi ya kukusanya ushuru wa maegesho ya magari, iliyokua chini ya Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (Tarura) irudishwe kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Waziri Bashungwa ametoa maagizo hayo hapo Jana  wakati wa Kikao chake na Uongozi wa Tarura na mawakala wa ukusanyaji ushuru wa maegesho kwenye halmashauri mbalimbali nchini.

Amesema kuwa, naona malalamiko kutoka kwa wananchi hayaishi kuhusiana na chanzo hiki  na Rais wetu Mhe. Samia Suluhu Hassan hafurahishwi na malalamiko haya ya wananchi kila mara na kuwataka Tarura wazidi kufanya Kazi Yao kiumahili zaidi.

Pia ameeleza kuwa, hili la ukusanyaji wa parking sio jukumu la msingi la Tarura, hivyo nalirudisha halmashauri, ili ninyi Tarura mkasimamie kutengeneza barabara na miundombinu mbalimbali katika jamii.

"Nataka kuazia Sasa Tarura iweze kufanya Kazi yake Kwa umahili wa Hali ya juu sitaki Tena wananchi walete malalamiko kuhusu suala nzima la miundo mbinu hivyo nataka halmashauri iweze kusimamia vinzuri suala nzima la ushuru na Tarura ifanye Kazi ya miundo mbinu tu". Amesema

Pia amemuelekeza Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Prof. Riziki Shemdoe kusimamia makabidhiano ya chanzo hicho haraka baina ya Tarura na Mamlaka za Serikali za Mitaa

Ameongeza kuwa: “Nitapenda kuona sasa Tarura mkielekeza nguvu kwenye kuimairisha miundombinu ya barabara za mijini na vijijini na mkafungue barabara na kufika kusikofikika, madaraja yakajengwe, makalavati ili kurahisha usafiri kwa wanannchi wetu,” amesema.

No comments