TBS WAKUTANA NA WAZALISHAJI WA MATOFALI ILI KUBORESHA VIWANGO VINAVYOKIDHI.
Akizungumza leo jijini Dar es salaam wakati wa
ufunguzi wa mkutano kati ya TBS na wasafirishaji wa bidhaa za nje ya nchi,
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, Mhandisi Johaness Maganga amesema kuwa
wao wana jukumu la kutoa mafunzo na ushauri viwandani juu ya uzalishaji wa
bidhaa bora.
Amesema kuwa jukumu lingine pia ni
kupima na kuhakiki vipimo vinavyotumika viwandani pamoja na kuelimisha umma juu
ya masuala yote yanayohusu uwekezaji na usimamizi wa viwango pamoja na udhibiti
wa ubora wa bidhaa.
Katika hatua nyingine Mhandisi Maganga amesema
kuwa TBS itaendelea kuandaa mikutano mbalimbali kwa wazalishaji wa bidhaa
mbalimbali hapa nchini lengo likiwa ni kujenga uelewa kuhusu umuhimu wa
kuzalisha bidhaa zinazokidhi matakwa ya viwango.
Pamoja na hayo TBS inatoa huduma ya upimaji wa
matofali kwenye parameter ya ” Frost weathering action” kwani ni eneo ambalo
wanunuzi wa matofali hutaka kujihakikisha kabla ya kujenga maeneo yenye maji
mengi.
Post a Comment