TMA ILIVYOKUSUDIA KUBORESHA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YAO.
NA NOEL RUKANUGA
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof.
Makame Mbarawa amewapongeza Wafanyakazi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania
(TMA) kwa
kuendelea kufanya kazi vizuri na kutekeleza majukumu kwa ufanisi mkubwa licha changamoto
mbalimbali zinazowakabili katika utekelezaji wa majukumu yao.
Akizungumza leo Aprili 21, 2022 Jijini Dodoma wakati akifungua kikao cha
Baraza la Wafanyakazi wa TMA. Waziri Pro. Mbarawa, amesema kuwa Mabaraza ya Wafanyakazi yameanzishwa kisheria kwa
lengo la kuwashirikisha wafanyakazi katika shughuli mbalimbali za utendaji wa
Taasisi.
“Nimejulishwa kwamba
mmekuwa mkitekeleza vyema takwa la kisheria, hivyo nawapongeza sana. nimefurahi
kusikia kwamba Baraza hili lina wajumbe kutoka vituo vyote vya Hali ya Hewa
Tanzania Bara na Zanzibar kwa kuzingatia muundo wa mkataba wa Baraza lenu”
amesema Prof. Mbarawa.
Amesema kuwa hali hiyo
inaonesha jinsi mawazo wafanyakazi kwa
pamoja yanavyotumika katika kuboresha huduma mnazotoa na kupelekea mafanikio
makubwa ambayo mnaendelea kuyapata ikiwa ni pamoja na kuendelea kumiliki cheti
cha ubora ISO 9001:2015.
Amesema Wizara
yake iko tayari kuwasaidia endapo kutatokea changamoto yoyote katika
utekelezaji wa jukumu ikiwemo ukusanyaji wa mapato.
“Hata hivyo, kuna jambo ambalo
nadhani ni vizuri mkalifamu na kulifanyia kazi.Majadiliano yenu yajikite
kuwaelimisha wadau kuitekeleza Sheria.Kuchangia huduma ni suala la kisheria
hivyo kila mdau hana budi kulitekeleza,” amesema Prof. Mbarawa.
Prof.Mbarawa ameitaka Mamlaka
hiyo iainishe bajeti na njia za ukusanyaji wa mapato ili
kuiwezesha taasisi kujiendesha kwa ufanisi.
“Natambua Serikali ni mdau mkubwa
katika huduma zitolewazo kwa jamii (Public Good), wakati Serikali inatekeleza
jukumu hilo wadau wanaotumia huduma kibiashara nao pia watekeleze wajibu wao wa
kuchangia huduma,” amesema.
Kuhusu changamoto ya maslahi duni
ya wafanyakazi, Prof. Mbarawa amesema Wizara kwa kushirikiana na
Ofisi ya Rais – UTUMISHI inalishughulikia suala hilo ambapo
ameahidi taratibu zikikamilika maslahi ya watumishi ikiwemo mishahara
itaboreshwa.
Ameeleza kuwa amefurahi kusikia
kuwa wapo katika hatua mbalimbali za majadiliano ya kukubaliana Tozo
mpya kwa sekta nyingine.
“Mmetoa mfano wa sekta ya Ujenzi,
Kwenye maji kwa maana ya wale wanao miliki vyombo, na watalii; ambao hawajaanza
kuchangia, na kwamba majadiliano yanaendelea vizuri. Nawapongeza sana katika
jitihada hizi,” amesema Prof. Mbarawa.
Mwenyekiti wa Baraza la
Wafanyakazi wa Mamlaka ya hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dkt. Agnes Kijazi ambaye
ni Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo, amesema kuwa Mamlaka imehakikisha
viwango na taratibu za kimataifa za utoaji wa huduma za hali ya hewa pamoja na
usimikaji wa vifaa na mitambo vinazingatiwa.
Amefafanua kuwa kwa mujibu
wa sheria, Mamlaka inafanya udhibiti wa shughuli kuu tatu ambayo ni uangazi wa
hali ya hewa (meteorological observation), utabiri wa hali ya hewa (weather and
climate forecasting) pamoja na kubadilisha mwenendo wa hali ya hewa (weather
modification).
Amesema kuwa
wamefanikiwa kuendelea kumiliki
Cheti cha utoaji huduma bora ISO 9001:2015 ambapo katika ukaguzi wa kimataifa
uliofanyika mwaka jana Disemba, 2021 Mamlaka ilifanya vizuri katika ukaguzi huo
na hakukuwa na hoja ya ukaguzi (Non – Confirmity).
Amesema kuwa wanaendelea na taratibu za ununuzi wa Rada nne (4) za hali ya hewa
zitakazofungwa katika Mikoa ya Mbeya, Kigoma, Dodoma na Kilimanjaro.
“Malipo ya awali
yameshafanyika na Rada hizo zinaendelea kutengenezwa huko Marekani. Rada hizo
zinatarajiwa kufungwa kati ya mwezi wa Julai, 2022 na Juni, 2023, ukamilishaji
wa mtandao wa Rada za hali ya hewa utasaidia utoaji wa huduma kwa Umma na kwa
sekta binafsi na pia kuboresha na
kupunguza madhara yanayotokana na hali mbaya ya hewa na hivyo kukuza uchumi wa Taifa letu” amesema
Dkt. Kijazi.
Ameeleza kuwa TMA imendelea kuiwakilisha nchi katika nyanja za kimataifa
zinazohusiana na masuala ya hali ya hewa.
na katika kipindi hiki tangu Baraza lililopita, pamoja na changamoto
za UVIKO-19, TMA imefanikiwa kutekeleza vyema jukumu lake la kuiwakilisha nchi
katika masuala ya hali ya hewa kikanda na kimataifa.
Amefafanua kuwa wataalamu
mbalimbali wa Mamlaka wameteuliwa na wameendelea kutekeleza majukumu yao katika
vikosi kazi mbalimbali vya Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO).
lengo la baraza hilo ni kupitia
bajeti ya Mamlaka ya mwaka 2022/2023 na kufanya tathmini ya utendaji wa
Mamlaka. Hii itasaidia kuongeza ubora na ufanisi katika utoaji wa huduma kwa
umma kwa lengo la kupunguza athari za mabadiliko ya hali ya hewa na tabia nchi.
Dk.Kijazi amsema kuwa Mamlaka
imehakikisha viwango na taratibu za kimataifa za utoaji wa huduma za hali ya
hewa pamoja na usimikaji wa vifaa na mitambo vinazingatiwa.
“Kuidhinishwa kwa Muundo wa
Taasisi na Miundo ya Maendeleo ya Watumishi (Schemes of Services). Muundo wa
Mishahara bado unaendelea kufanyiwa kazi,” amesema.
Pia, kuendelea na taratibu za
ununuzi wa Rada nne za hali ya hewa zitakazofungwa katika Mikoa ya
Mbeya, Kigoma, Dodoma na Kilimanjaro.
“Malipo ya awali yameshafanyika
na Rada hizo zinaendelea kutengenezwa huko Marekani.Rada hizo zinatarajiwa
kufungwa kati ya mwezi wa Julai, 2022 na Juni, 2023,”amesema.
Amesema kuwa TMA inakabiliana na
changamoto ya maslahi madogo ya watumishi hali inayopelekea wataalamu
kuhamia katika Taasisi zingine.
Post a Comment