COSTECH YAJA NA MKAKATI MPYA WA MAWASILIANO.
Hayo yalibainika wakati wa warsha uandaaji wa Mwongozo wa Utekelezaji Mkakati wa Mawasiliano, iliyofanyika kuanzia tarehe 19 – 23 Aprili 2022 na katika ukumbi Kituo cha Hisabati, uliopo Chuo cha Ualimu, Morogoro (MOTCO).
Meneja Utunzaji Nyaraka na Machapisho kutoka COSTECH, Dkt. Bunini Manyilizu anafafanua kuwa katika warsha hiyo, kikosi kazi kilijadili Mwongozo huo na kuja na rasimu itakayohusianisha na Mpango wa Mawasaliano ambao umeandaliwa kwa kipindi cha miaka mitatu na inatarajiwa kutumika kuanzia mwaka 2023 -2026.
Dkt.Manyilizu amewataka wananchi na wadau mbalimbali wa mawasiliano kufuatilia taarifa za kielektroniki katika vyanzo vya kisayansi na kiteknolojia vinavotambulika.
Afisa Uhusiano kutoka COSTECH Bw. Faisal Abdul anafafanua zaidi. “Kupitia muongozo huu Tume itaongeza tija ya kujitangaza kwa kuwa karibu wadau muhimu kama vyombo vya habari ili kusaidia kufikia lengo na utekelezaji wa jukumu la taasisi katika kuhifadhi, kuchakata na kusambaza taarifa za Sayansi Teknolojia na Ubunifu nchini, alisema Bw. Abdul.
Naye mratibu wa warsha hiyo Bi. Minza Charles alisema kuwa amejifunza mengi kupitia warsha hii na kupata uzoefu kutoka taasisi nyingine hapa nchini.
Post a Comment