Ads

RAIS SAMIA SULUHU APOKEA TAARIFA YA TAKUKURU PAMOJA NA HESABU ZA SERIKALI KWA MWAKA 2020/2021

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Taarifa ya Taasisi ya TAKUKURU kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo CP Salum Hamduni katika hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Jijini Dodoma leo tarehe 30 Machi, 2022. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Taarifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2020/2021 kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) Charles Kichere katika hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Jijini Dodoma leo tarehe 30 Machi, 2022. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali mara baada ya kupokea Taarifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2020/2021 pamoja na Taarifa ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU, katika hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Jijini Dodoma leo tarehe 30 Machi, 2022. 

Viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla ya uwasilishwaji wa Taarifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2020/2021 pamoja na Taarifa ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU katika hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Jijini Dodoma leo tarehe 30 Machi, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka Watendaji wa Serikali kufanya kazi kwa weledi badala ya kukimbilia kupandishwa  vyeo bila kuvifanyia kazi.
Rais Samia amesema hayo leo  alipokuwa akizungumza baada ya kupokea ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)  na TAKUKURU, Jijini Dodoma.
Aidha Rais Samia amewataka Wabunge katika maeneo yao kuwaeleza wananchi  kuhusu mambo yanayoendelea kimataifa, mfano vita ya Ukraine na Urusi ambavyo vimechangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la bei ya mafuta na kusababisha  bidhaa kupanda bei.
Pamoja na hayo Rais samia ameagiza tozo ya shilingi 100 iliyokuwa imetolewa kwenye mafuta irejeshwe kwa sababu hesabu zake tayari zilikuwa zimepigiwa kwenye bajeti na amesema kuwa kwa mwenendo wa upandaji wa bei ya mafuta duniani kuondoa Shilingi 100 hakutasaidia, ila kutainyima serikali mapato.
Kwa upande wake  Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Salum Hamduni amesema taasisi hiyo kwa kushirikiana na ofisi ya Taifa ya Mashtaka imeweza kutaifisha mali za Sh1.2 bilioni, pia Takukuru imeweka zuio la fedha Sh400.5 milioni pamoja na mali zenye thamani ya Sh2.6bilioni. Mali hizo ni nyumba 15, viwanja viwili na magari matatu 

No comments