Ads

Urusi na China zalaani vikwazo vya Magharibi dhidi ya Moscow kuhusu Ukraine

 


Mawaziri wa Mambo ya Kigeni wa Urusi na China leo wamelaani kile walichokiita vikwazo vya Magharibi visivyo halali na visivyokuwa na tija, ambavyo vimewekwa dhidi ya Moscow kuhusiana na uvamizi wake nchini Ukraine.

 Waziri wa Mambo ya Kigeni wa China Wang Yi amefanya mazungumzo na mwenzake wa Urusi Sergei Lavrov katika mkoa wa mashariki mwa China wa Anhui, ambako China inatarajiwa kuwa mwenyeji wa mikutano ya siku mbili kuhusu Afghanistan.

 Urusi inatafuta uungwaji mkono wa China na ushirikiano wakati ikiendelea kutengwa kutoka mifumo ya kimataifa ya kifedha na usambazaji bidhaa zake.

 Nchi hizo mbili zimekubaliana kuendelea kuimarisha ushirikiano wao wa kimkakati na kuyazungumzia masuala ya kimataifa kwa sauti moja.

credit DW

No comments