Ads

MAJI CHINI YA ARDHI KWA UCHUMI NA VIWANDA

 Imeelezwa kuwa maji ya asili yaliyohifadhiwa kwenye miamba ya ardhi au yanayotiririka kwenye miamba ya ardhi yanaweza kutegemewa katika shughuli za kijamii na ustawi wa jamii kwa ujumla.

Mshuda Wilson Mhaidrojiolojia Mwandamizi amesema sehemu nyingi ambazo hazina mito wala mabwawa, hutegemea zaidi maji ya ardhini.

Amesema kitakwimu maji baridi tuliyonayo duniani ni kidogo sana."Pamoja na kwamba karibu 70% ya dunia imefunikwa na maji, ni 2.5% tu ya maji hayo ni baridi na 97.5% miya chumvi ambayo hayafai kwa matumizi ya binadamu.

 "Kati ya hiyo 2.5% ya maji baridi, 70% yapo kwenye mifumo ya barafu iliyopo Arctic, Antartica na Greenland "

Mshuda Wilson Mhaidrojiolojia mwandamizi amesema kuwa asilimia 30 ya 2.5% ni maji yanayojumuisha unyevunyevu uliopo kwenye udongo, mvuke ulioko angani na maji yaliyoko kwenye mito, maziwa na mabwawa. 

"30% ya 2.5% ni 1/3 tu ya maji haya ndio yanapatikana katika mito, maziwa na katika kina kifupi chini ya ardhi na hivyo kuweza kutumiwa na binadamu."

Amesema kuwa kiasi cha maji yanayofaa kwa matumizi ya binadamu Tanzania kwa sasa ni kilomita za ujazo 89 sawa na mita za ujazo 2,700 kwa mtu kwa mwaka. 

Amesema kuwa kufikia mwaka 2025 kiasi hiki cha upatikanaji wa maji kwa mtu kwa mwaka kitapungua kwa 45% na kufikia mita za ujazo 1,500, ikiashiria kwamba wakati huo patakuwepo na uhaba wa maji, kwani kiasi cha maji chini ya mita za ujazo 1,700 kwa mtu kwa mwaka ni kiwango kinachoonesha kuwa kuna uhaba wa maji.

"Kutokana na ukweli huo ndio maana Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kuwa watanzania wanaendelea kupata maji safi na salama.

"Wote tunajua kuwa ndani ya kipindi cha mwaka mmoja tu wa utawala wake, amenunua mitambo mikubwa ya kisasa ya kuchimba visima virefu kwa kila mkoa; si hivyo tu, amenunua vifaa vipya na vya kisasa vya utafiti wa maji ya ardhini, vifaa vipya na vya kisasa vya upimaji ubora wa maji”

"Hivyo, naamini pamoja na kuwa tafiti zinaonesha kuwa kufikia mwaka 2025 tutakuwa tunapata maji kiasi cha mita za ujazo 1,500 kwa mtu kwa mwaka ila kwa juhudi hizi maji yataendelea kupatikana kwa kiwango kinachohitajika kwa mtu kwa mwaka. "

Mshuda Wilson Mhaidrojiolojia amesema anachokiomba kutoka kwa kila mtanzania ni kutoa ushirikiano wa karibu katika utunzaji wa vyanzo vya maji.

Chanzo cha maji ya mto wakati wa kiangazi. Mshuda Wilson Mhaidrojiolojia amesema vile kipindi cha kiangazi hakuna mvua yoyote inayonyesha, hivyo maji yote yanayotiririka mtoni huwa yanatokana na maji ya ardhini ambayo hutokeza kama chemichemi mahala fulani na chemichemi moja zikiungana na chemichemi nyingine mwisho wake hutengeneza kijito.

Mhaidrojiolojia huyo amesema  kijito kimoja kikiungana na kijito kingine hatimaye hutengeneza mto ambao hutiririka mpaka ziwani au baharini.

Chanzo cha maji ya ardhini maji ya ardhini hutokana na kutuama kwa maji ya mvua ambapo mvua inaponyesha baadhi ya maji hutuama ardhini. Hali hii imeelezewa vizuri kwenye mzunguko wa maji (water cycle) ambao hufundishwa mashuleni kwenye somo la jiografia. 

Amesema mzunguko huo huanza kwa jua kuwaka na kutengeneza mvuke ambao hupanda juu na mwisho hutengeneza mawingu ya mvua.

Amesema mawingu hayo huendelea kuganda na mwisho wake hushuka chini kwa mfumo wa mvua, baada ya mvua kutua chini baadhi ya maji hutuama ardhini na mengine hutiririka kwenye vijito ambacho mwisho wake huungana na kijito kingine na kutengeneza mto ambao hutiririka mpaka baharini au ziwani.  

Maji yanayotuama ardhini hutengeneza mkondo wa maji chini ya ardhi (Aquifer) ambao mwisho wake hutokeza kwenye uso wa ardhi kwa mfumo wa chemichemi, baadhi ya chemichemi huendelea kutiririsha maji hata wakati wa kiangazi na ndio huwa chanzo cha maji ya mto wakati wa kiangazi.

Wakati mto unapotiririsha maji yake wakati wa kiangazi kwa kawaida huendelea kutuamisha maji maeneo mengine ambayo hayana chemichemi na kuingia kwenye mikondo ya maji ya ardhini (aquifer). 

Kulingana na hali hiyo  hivyo, kuchafuliwa kwa maji ya kijito au mto kutokana na takataka ngumu yoyote ile husababisha kuchafuliwa kwa maji ya ardhini ambayo kimsingi ndo huwa tegemeo la walio wengi kwa kizazi cha leo nacha baadae.

Mshuda Wilson Mhaidrojiolojia amesema kuwa utunzaji, mipaka ya kihaidrolojia. Mfano Bodi ya maji Bonde la Wami Ruvu inapita kwenye mikoa sita ambayo ni Manyara kidogo (Kiteto), Tanga kidogo (Handeni na Pangani), Dodoma, Morogoro, Pwani na Dar es salaam yote.

Amesema Jumla ya wilaya 27 zimo ndani ya bodi hilo; Bodi ndo ina jukumu la kugawa rasilimali hii muhimu na adimu kwa kuzingatia sera ya maji ya mwaka 2002 na sheria ya UTUNZAJI WA RASILIMALI ZA MAJI Na. 11 ya mwaka 2009.

Sera ya maji imetoa kipaumbele katika ugawaji huo wa maji. Kutokana na sera ya maji kipaumbele cha kwanza nikwa ajili ya matumizi ya umma ikifuatiwa na mahitaji ya mazingira kwa viumbe vinavyoishi majini na mwisho nikwa mahitaji ya maendeleo ya kiuchumi (Social Economic Activities).

"Kutokana na vipaumbele hivyo, ndio maana inapotokea kupungua kwa Rasilimali hii kama ilivyotokea mwaka jana, ndipo Bodi huchukua maamuzi ya kusitisha vibali vingine na kubakiza kibali cha mamlaka ya usambazaji maji kama DAWASA kama ilivyotokea mwaka jana mwishoni. "

Hayo yanafanyika kwa mujibu wa kifungu cha 49(1) cha sheria ya maji.  Katika kutimiza majukumu yake ya Kulinda na kusimamia Rasilimali hii ya maji, Bodi imeendelea kutoa huduma zifuatazo:-Kutoa vibali vya uchimbaji visima kwa mujibu wa sheria (kifungu Na. 54(1) cha Sheria ya maji)Kutoa vibali vya utiririshaji wa maji taka kutoka viwandani na sehemu mbalimbali kwa mujibu wa kifungu Na. 63(1) cha sheria ya maji. 

Kutoa ushauri wa kitalaam kwa mtu yeyote anayetaka kuchimba kisima , "Hii inatokana na ukweli kuwa baadhi ya visima viko karibu sana na mashimo ya maji taka kitu ambacho hakishauriwi kitaalam kupiga faini kwa watu wanaokiuka na kuvunja sharia kwa mujibu wa kifungu 55(2) ya sheria ya maji."

UMUHIMU WA MAJI YA ARDHINI KATIKA MAENDELEO YA UKUAJI UCHUMI

Inaelezwa kuwa kwa vile uzalishaji wa bidhaa wowote ule utegemea maji, nakwa vile ukuaji wa uchumi wa taifa lolote hutegemea zaidi uzalishaji wa viwanda .

"Ni Dhahiri kuwa viwanda hivyo hutegemea maji ya ardhini katika uzalishaji wa bidhaa. hii inatokana na viwanda vingi kuhitaji maji mengi wakati wa uzalishaji bidhaa."

Amesema hii maana yake ni kwamba utunzaji mathubuti wa vyanzo vya mahi huenda sambamba na dhana nzima ya ukuaji wa uchumi wa viwanda au Tanzania  ya Viwanda.

Amesema tunapokuwa tunaendelea na wiki ya maji ambayo husherehekewa kila mwaka kipindi kama hiki, Bodi ya maji Bonde la Wami Ruvu inatoa ( offer ) kwa wateja wake watakaojitokeza kuomba vibali vya utumiaji maji bila kulipa adhabu ya kutokuomba kibali kabla ya uchimbaji kisima.

Anasisitiza kuwa  "Kwa wachimbaji tunatoa vibali vya uchimbaji bure wakati wa kipindi hiki cha wiki ya maji, Tunatoa wito kwa mtu yeyote atakayeona mashine inachimba bila kibali cha uchimbaji. Ofisi itatoa zawadi kati ya Tsh 50,000 na Tsh 100,000 papo kwa papo kwa mtu atakayefanikisha kupatikana kwa mashine inayofanya kazi ya uchimbaji bila ya kuwa na kibali cha uchimbaji ."

Jamii imeshauriwa kutokubali  kuingia gharama kubwa ya kuchimba kisima bila ya kufanya upimaji wa kisima. 

Hii itakusaidia kuelewa mambo yafuatayo:-Wingi wa maji Ubora wa majiChangamoto utakazokutana nazo kwenye kisima chako.

Gharama za upimaji zimeelezwa kuwa ni Tsh 300,000 kwenye miamba laini kama ya Dar es salaam na Tsh 1,500,000 kwenye miamba migumu kama morogoro na maeneo mengine. 

Tofauti ya gharama hizi inasababishwa na aina ya mashine zinazotumika kwenye upimaji na namna ya upimaji wenyewe kutegemea na upatikanaji wa maji ya ardhini.Ndugu mchimbaji epuka kupigwa faini ya kupeleka mashine kuchimba mahali ambapo hakuna kibali cha uchimbaji.

Faini kwa mashine ambayo haina kibali cha uchimbaji ni kubwa sana wakati kibali cha uchimbaji kinagharimu kiasi cha Tsh 150,000 tu.

Ombi kwa wenye viwanda wanaotumia maji ya visima kutoa ushirikiano wa karibu kwa malipo ya utumiaji maji ya visima.

Ambapo imeelezwa kuwa  kimsingi bodi inafanya hivyo ili kuhakikisha biashara yenu haikwami kwa namna yoyote ile kwa kuhakikisha kuwa maji safi na salama yanapatikana ardhini kwa ajili ya matumizi ya uzalishaji bidhaa.

No comments