Ads

MAZUNGUMZO NA MASHARTI YA URUSI KUMALIZA VITA NCHINI UKRAINE

 


Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Mevlut Cavusoglu amefanya kikao cha mazungumzo na waziri wa mambo ya nje wa Russia, Bw. Sergey Lavrov na Waziri wa ukraine Bw. Dmytro Kuleba.

Huyo unayemuona katikati ya picha ndo Waziri wa Uturuki Mevlut Cavusoglu, kushoto kwake ni waziri wa Russia Sergey Lavrov na kulia kwake ni waziri wa Ukraine Dmytro Kuleba.

Waziri wa uturuki ambaye alikuwa anatumika kama msuluhishi alisema kwamba mazungumzo yanaendelea vizuri na kuna dalili kubwa za mafanikio.

Kuna Mambo Sita makubwa ambayo yanazungumzwa kwa undani kabisa na kama yatafanikiwa basi vita hii itakuwa imekwisha. Mambo hayo 6 ni kama yafuatavyo:

1. Ukraine Kutojiunga na Umoja wa Ulaya na NATO (Ukraine Neutrality).


2. Uhakika wa Masuala ya Ulinzi na kutotumia nguvu za Kijeshi.


3. Kuwaondoa viongozi wa Ukraine ambao ni vibaraka wa Ulaya na Marekani (De-Nazification).


4. Kuondoa vikwazo na ulazima wa kutumia lugha ya Russia katika nchi ya Ukraine.


5. Kutafuta suluhu ya msuguano wa kimaslahi katika ukanda wa Donbas.


6. Kutafuta maelewano na kujadili mzozo wa kuchukuliwa kwa Peninsula ya Crimea wa mwaka 2014.


Mazungumzo haya yalifanyika katika mji wa Antalya nchini Uturuki. Kuisha kwa mazungumzo haya ndo kulimnyanyua Rais wa Ukraine Bw Volodymyr Zelenskyy na kumuomba Putin mazungumzo ya amani.


"Huu ni muda muafaka wa kukutana, kuongea yote ambayo yanapaswa kuwekwa sawa, naomba tukae mezani na kuweka sawa mambo yote ambayo yanaumiza raia wa Ukraine".




No comments