WAZIRI WA MADINI DKT. BITEKO AFUNGUA MAONESHO YA NNE YA KIMATAIFA YA UWEKEZAJI KATIKA SEKTA YA MADINI.
Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko pamoja na Waziri wa Nishati na Madini wa Burundi, Ibrahimu Uwizeye wamezindua maonesho ya kimataifa ya madini yanayoendelea katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere ikiwa ni sehemu ya mkutano wa kimataifa wa uwekezaji katika sekta ya madini unaotarajiwa kuanza mapema kesho tarehe 22 Februari, 2022.
Akizungumza mara baada ya kutembelea mabanda kwenye maonesho hayo, Waziri wa Nishati na Madini wa Burundi, Ibrahim Uwizeye amepongeza maandalizi na kufafanua kuwa nchi ya Burundi inaendelea kujifunza kuhusu usimamizi kwenye Sekta ya Madini Tanzania
Waziri wa Madini Dkt. Doto
Biteko (Katikati) pamoja na Waziri wa Nishati na Madini wa Burundi, Mhe. Ibrahimu
Uwizeye wakikata utepe wa uzinduzi wa Maonesho ya Nne ya Kimataifa ya Uwekezaji katika
Sekta ya Madini yanayofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu
Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam ambapo yanatarajiwa kuanza mapema
kesho Februari 22 hadi 23 mwaka huu.
Waziri
wa Madini Dkt. Doto Biteko pamoja na Waziri wa Nishati na Madini wa Burundi,
Mhe. Ibrahimu Uwizeye wakitembelea banda la Kampuni ya FARU Graphite
Corparation katika Maonesho ya Nne ya Kimataifa ya Uwekezaji katika Sekta ya
Madini yanayofanyika katika Ukumbi wa
Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya wadau katika sekta ya madini wakitembelea banda la Tume ya Madini katika
Maonesho ya Nne ya Kimataifa ya Uwekezaji katika Sekta ya Madini yanayofanyika katika
Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es
Salaam.
Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko akizungumza jambo na Waziri wa Nishati na Madini wa Burundi, Mhe. Ibrahimu Uwizeye katika Maonesho ya Nne ya Kimataifa ya Uwekezaji katika Sekta ya Madini yanayofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.
Post a Comment