Ads

Wachezaji watatu AZAM wasimashwa , kwa muda usiojulikana.

 WACHEZAJI watatu wa Klabu ya Azam FC ambao ni Nahodha Aggrey Morris, Nahodha Msaidizi Salum Abuubakar (Sure Boy) pamoja na  Kiungo Mudathir Yahya Abbas wamesimamishwa kwa muda usiojulikana kutokana na utovu wa nidhamu.


Taarifa ya Azam FC iliyotolewa leo Oktoba 6,2021 imesema kwamba wachezaji hao wameonesha utovu wa nidhamu kwa Meneja wa timu, Wachezaji wenzao, Benchi la Ufundi na Viongozi wa Klabu kwenye vyumba vya kubadilishia nguo.

Katika taarifa hiyo iliyotolewa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Klabu hiyo, Thabit Zacharia amesema wachezaji hao walimfuata Ofisini kwake Meneja wa Klabu, Luckson Kakolaki na kumtolea maneno yasiyo na staha Septemba 18, 2021 siku ya mchezo wa pili wa raundi ya awali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Horseed FC ya Somalia.

Amesema kuwa taratibu za nidhamu zilifuatwa na uongozi wa Klabu kupitia Kamati yake ya Nidhamu, kuwasililiza wachezaji hao, ambapo ilibainika maelezo yao ya utetezi yalikosa mashiko mbele ya Kamati hiyo na adhabu hiyo kuendelea pale pale.


 Nahodha Mkuu wa Azam FC, Aggrey Morris (Pichani) ambaye amesimamishwa na Uongozi wa Klabu hiyo na Wachezaji wengine Salum Abubakar na Mudathir Yahya.

No comments