DKT. JINGU: WANAUME WANATAKIWA KULIDHISHWA NA WANAWAKE WANAOKUZA UCHUMI WA FAMILIA.
Na Francisco Peter, Dar es Salaam.
Wanawake wametakiwa kushiriki katika utekelezaji wa shughuli za kiuchumi katika jamii jambo ambalo litasaidia Taifa kusonga mbele katika nyanja mbalimbali za kimaendeleo.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Afya Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. John Jingu katika ufunguzi wa kikao na Wanawaasisi wa Umoja wa Jumuiya za Wanawake katika nchi huru za Afrika (PAWO).
Amesema kuwa serikali inajua wanawake walipotoka na wanapokwenda, huku akisisitiza wanaume wanapaswa kulidhishwa na hali ya wanawake wanapokuwa wanapambania uchumi katika familia zao.
Ameeleza kuwa madhumuni ya umoja huo ni kuunganisha wanawake wa Afrika ili kuleta usawa, maendeleo na amani.
Mwenyekiti wa PAWO Tawi la Tanzania Mama Leah Lupembe, amesema kuwa umoja huo ulianzishwa rasmi Julai 31,1962 na viongozi wachache wa Afrika.
"Kilianzishwa wakati wa miaka ya kupigania uhuru, waliona matatizo ya wanawake yanafanana, hivyo wawe na chombo cha kuzungumza ili kutatua chngamoto zetu” matatizo"amesema Mama Leah.
Katibu wa PAWO Dkt. Susan Alphonce Kolimba amesema wapo katika nchi 25, ambapo Katibu wa Tanzania ni mtendaji katika Afrika Mashariki tangu kuanzishwa kwake ili kutetea wanawake wote wa Afrika.
Amefafanua nchi ya Tanzania kupitia Wizara ya afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto kuwa ni watendaji katika PAWO kwa muda wa miaka mine, PAWO ni wadau katika wizara hiyo na wanakuwa wanazungumzia mbambali ikiwemo kuangalia namna ya kutatua changamoto.
Post a Comment