KAMISHNA WA BIMA AWASISITIZA MAWAKALA WA BIMA KUTOA ELIMU KWA WANANCHI.
Na Francisco Peter.
Mawakala na Makampuni ya Bima kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wametakiwa kuwekeza nguvu katika kutoa elimu kwa jamii ili kufikia malengo ya serikali ya kufikia asilimia 80 ya wananchi kuwa uelewa kuhusu masuala ya bima pamoja kufikia asilimia 50 ya watanzania wawe wamepata hadi kufikia mwaka 2030.
Akizungumza jijini Dar es Salaam Kamishna wa Bima Bw. Mussa Juma wakati akifungua Mafunzo ya siku mbili yaliyoandaliwa na Chama Cha wakala wa Bima Nchini kwa lengo la kutoa elimu juu ya namma Bora ya kuendesha uwakala wa Bima, namna yakutafuta Masoko pamoja na kufahamu mambo ya kodi kuhusu Bima hatua ambayo itawasaidia wakala hao kufanya kazi Kwa ufanisi mkubwa.
Kamishna huyo wa bima kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Nchini (TIRA), amesema kwa ili kufikia malengo ya serikali ni muhimu mawakala, madalali pamoja na makampuni ya Bima kuendelea kutoa elimu Kwa wateja, kuuza bidhaa za Bima kulingana na uwezo wa kampuni zao pamoja na kushughulikia na kutatua kwa haraka migogoro ya bima inayojitokeza Kwa wateja wao.
"Kujiendeleza kielimu inasaidia kuwa nauelewa Mpana katika masuala ya Bima hususani mambo ya teknolojia na hii inawasaidia msiachwe nyuma kwenye ushindani,hivyo jitahidini Kila mmoja awe na kitu cha kipekee ili unaeshindana nae asiweze kukushinda ,kwahiyo mnapata semina hii kuwafanya msitupwe kwenye ushindani"amesema.
Mwenyekiti wa Chama Cha wakala wa Bima Nchini Bw.Sayi Jonh Daudi ameiomba serikali kuondoa sharti la kuwekea kiwango cha fedha benki (FDR) ambacho kitatumiwa na wakala kulipa gharama za bima pindi atakapokutana na changamoto za kutenda nje ya utaratibu kwa mteja wake nakwamba sharti hilo limekuwa kikwazo Kwa wakala wa bima ambao ni wapya.
"Tunaiomba serikali iondoe hiki kigezo kinachomtaka mtu anaetaka kutoa huduma za bima lazima awe na kiasi Fulani cha fedha benki ambacho kinaweza kutumika kumlipa mteja anaetendewa kinyume cha utaratibu, jambo hili limekua kikwazo kikubwa Kwa wakala wa bima,tunaiomba ikiwezekana waiondoe " amesema Bw.Sayi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Bima ya FIDES Insuarence iliyopo Dar es salaam.
Baadhi ya viongozi watendaji wa makampuni ya wakala wa Bima akiwemo Bi.Modesta Liviga wa Kampuni ya Primode Insuarence Agence. pamoja na Bw.Meshaki Matulile mtendaji mkuu wa Kampuni ya BMC Insuarence Agence. wamesema Kwa nyakati tofauti kuwa Mafunzo hayo yatawasaidia kufahamu namna nzuri ya kuuza bidhaa za bima,kutafuta Masoko ya Bima hatua ambayo itasaidia kufanya kazi zao Kwa ufanisi mkubwa.
Mwenyekiti wa Chama hicho Sayi John Daudi amesema kwa siku za
usoni wanafikiria kuwa na mawakala wa bima ambayo lengo itakuwa kuonesha UMMA
shughuli wanazo zifanya.
Mkurugenzi wa Mafunzo kutoka Kampuni ya First Assurance Amour Abbas iliyopo Jijini Dar es Salaam na baadhi ya mikoa mingine ya Mbeya , Morogoro , Tanga, Mwanza na Zanzibar akitoa mafunzo katika semina hiyo alisema wadau wawe na sifa ya ushawishi mkubwa katika ufanyaji kazi hali itakayo waletea faida zaidi.
Amesema kuwa First Assurance imeendelea kukua kutokana na jitihada na hivyo kupata kutanuka katika nyanja za kiuchumi na kuwashauri wadau wa makampuni ya Bima kuwa na malengo mazuri kukuza mafanikio yao .
"Napenda pia kuwashauri wadau ambao ni makampuni ya Bima kuendelea kuweka mipango mizuri ya kutoa Bima zaidi ya moja ," amesema Abbas. ambapo amewashauri makampuni ya hayo kufatengeneza agenti wengi.
Post a Comment