WAZIRI MKENDA ATUA BABATI//AITAKA NFRA KUFANYIA KAZI CHANGAMOTO KABLA YA KUKABIDHIWA MRADI WA VIHENGE VYA KISASA NA MAGHALA
Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda akikagua ujenzi wa maghala na vihenge vya kisasa vya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) wakati alipofanya ziara ya kikazi ya siku moja Wilaya ya Babati Mkoani Manyara leo tarehe 16 Agosti 2021. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda akikagua ujenzi wa maghala na vihenge vya kisasa vya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) wakati alipofanya ziara ya kikazi ya siku moja Wilaya ya Babati Mkoani Manyara leo tarehe 16 Agosti 2021.
Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda akipata maelezo ya ujenzi wa maghala na vihenge vya kisasa vya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) wakati alipofanya ziara ya kikazi ya siku moja Wilaya ya Babati Mkoani Manyara leo tarehe 16 Agosti 2021.
Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda akikagua mitambo ya kusafisha nafaka kwenye ujenzi wa maghala na vihenge vya kisasa vya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) wakati alipofanya ziara ya kikazi ya siku moja Wilaya ya Babati Mkoani Manyara leo tarehe 16 Agosti 2021.
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Manyara
Serikali imebainisha kuwa kuchelewa kukamilika kwa ujenzi wa
Vihenge vya Kisasa na Maghala kumetokana na tatizo la mgogoro wa mwingiliano wa
viwanja kati ya Shirika la umeme (TANESCO) na Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya
Chakula (NFRA).
Mgogoro huo ulipelekea mkandarasi kusimama na baadaye kuongezewa
muda wa mkataba wa kutekeleza mradi mpaka tarehe 13 Septemba 2021.
Akizungumza mara baada ya kufanya ziara ya kikazi ya siku moja
Wilaya ya Babati Mkoani Manyara leo tarehe 16 Agosti 2021 Waziri wa Kilimo Mhe.
Prof. Adolf Mkenda amesema kuwa pamoja na mradi huo kukamilika kwa asilimia
99.8 kama inavyotajwa lakini bado NFRA inapaswa kuzifanyia kazi changamoto
mbalimbali kabla ya kukabidhiwa mradi huo.
Waziri Mkenda amebainisha kuwa changamoto hizo ni pamoja na kupewa
elimu ya namna gani vihenge hivyo vitaweza kufanyiwa usafi kwani kwa sasa
hakuna uwezekano wa kufanya usafi jambo ambalo ni hatari kwa uhifadhi wa nafaka
zinazonunuliwa na kuhifadhiwa na serikali.
Pia ameitaka NFRA kuhakikisha kuwa inasimamia utekelezaji wa
uwezekano wa njia sahihi ya kutibu nafaka inayohifadhiwa kwenye Vihenge hivyo
vya kisasa (Fumigation) kwani eneo hilo ni muhimu zaidi kwa ajili ya uhifadhi.
Ujenzi wa Vihenge vya Kisasa na Maghala kanda ya Arusha
inayojumuisha mikoa ya Arusha na Manyara katika kituo cha Babati unatekelezwa
na kampuni ya Unia Sp.zo.o kutoka nchini Poland kwa kushirikiana na kampuni ya
wazawa ya Elerai Construction Company Ltd kwa gharama ya Dola za Kimarekani
Milioni 8.08 ambazo ni sawa na Bilioni 18.67 za kitanzania.
Kwa ujumla sehemu kubwa ya mradi imechukuliwa na ujenzi wa
vihenge ambao ni zaidi ya asilimia 60 ya mkataba.
Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kwa sasa una
maghala 34 yenye uwezo wa kuhifadhi nafaka Tani 251,000 katika kanda zake nane
za kimakakati.
Hivyo serikali inaendelea na utekelezaji wa mradi huo ambao ni maalumu kwa ajili ya kuongeza uwezo wa kuhifadhi kwa jumla ya Tani 250,000 wenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 55 ambazo ni sawa na Bilioni 126.5 ambapo mradi huo utakapokamilika utaongeza uwezo wa kuhifadhi wa NFRA kutoka Tani 251,000 za sasa hadi kufikia Tani 501,000.
Post a Comment