Ads

SIJUTII KUJIFUKIZA : DKT GWAJIMA

 


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Dorothy Gwajima amesema, hatajuii kitendo cha kujifukiza ikiwa ni sehemu ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa corona.


Dkt  Gwajima ameyasema hayo leo Agosti 16 2021 akiongeza kuwa hajutii pia kutumia dawa za asili kama ambavyo alionekana siku za nyuma akifanya hivyo kama njia mojwapo ya kujikinga na ugonjwa huo.

Amesema kuwa aliamua kutumia njia hizo za asili kutokana na ukweli kuwa tiba za asili zimethibitshwa na mamlaka husika na zinafanyika kwa mujibu wa sheria na taratibu huku akiwataka Watanzania kutokupotosha maelekezo aliyoyataoa aliyekuwa Rais wa awamu ya Tano hayati Dk John Magufuli.

"Kwa nini hamsemi kuwa Hayati (Magufuli) aliitaka Wizara ya Afya kujiridhisha kwanza kabla ya kuruhusu chanjo hizo? Yaani ninyi mnasema tu kwamba alisema chanjo ni mbaya, wakati alisema hivyo na kutoa angalizo kwamba kabla hazijaruhusiwa lazima wataalam wetu wajiridhishe na ubora wake na ndio kazi iliyofanyika kabla ya serikali ya awamu ya sita kuruhusu chanjo kuanza kutolewa," amesema Dk Gwajima.

Amesema kuwa wakati janga la corona linaingia nchini Aprili mwaka jana hakukuwa na namna ambavyo watu wangeweza kujikinga na ugonjwa huo kutokana na ukweli kuwa chanjo hazikuwepo duniani. 

No comments