RC MAKALA AAGIZA KUIMARISHWA ULINZI NA USALAMA
Baadhi ya wananchi waliojitokeza katika mkutano wa kusiliza kero ulioandaliwa na mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam.
Na John Luhende
MKuu wa Mkoa wa Dar es salaam mhe. Amos Makala amezitaka kamati za ulinzi na usalama mkoani Dar es salaam kuimarisha ulilinzi na usalama Katika Kila eneo la Mkoa huo ili kazi za maendeleo ziweze kufanyika kwa usalama.
Makala ametoa kauli hiyo na kuwatolea mwito Wenyeviti wa mtaa ,Madiwani na na mabalozi wa nyumba kumi kuwatambua watu wageni wote wanapoingia Katika maeneo ya utawala.
Aidha Makala amewataka wananchi wa Mkoa huo kuendelea kuchukua tahadhali ya ugonjwa wa CORONA na kuitumia haiari yao kuchanjwa.
Makala yupo Katika ziara ya kusikiliza kero za wananchi Katika majimbo ya Pembezoni mkoani humo amabapo awali akizunguma Katika ufunguzi wa kutano huo amewataka wananchi wa majimbo yaliyolengwa Katika ziara hiyo kujitokeza kwa wingi Katika mikutano hiyo.
Post a Comment