Ads

TECNO YATOA ZAWADI YA GARI MPYA KWA MTEJA WAKE.

 Mshindi wa gari mpya katika Promosheni ya 100 Million Vimba na Camon 17 na Spark 7 Bi. Sophia Suleiman akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam baada ya kukabidhiwa  zawadi ya gari.

Mshindi wa gari mpya katika Promosheni ya 100 Million Vimba na Camon 17 na Spark 7 Bi. Sophia Suleiman akikabidhiwa zawadi ya gari.
Gari Mpya.
Baadhi ya washiriki wa Promosheni wakiwa katika picha baada ya kupewa zawadi zao.

.............

Hitimisho la Promosheni ya 100 Million Vimba na Camon 17 na Spark 7 ilikuwa ni Tarehe 25/08 baada ya kumshuhudia Bi. Sophia Suleiman akiibuka mshindi wa zawadi ya gari mpya, na wengine kujishindia pikipiki na majokofu.

“Promotion hii imechukua takribani mwezi mmoja ambapo lengo lake lilikuwa ni kutoa shukurani zetu kwa wateja wa TECNO ambao wamekuwa nasi wa takribani miaka kumi, na kwa kipindi hiki tumeamua kutoa zawadi kubwa zaidi ya gari ikiwa kama heshima na kuthamini mchango wa wateja wetu” amesema William Motta mwakilishi wa Kampuni ya TECNO.  

Promosheni ya 100 Million Vimba na Camon 17 na Spark 7 ilizinduliwa rasmi mnamo Tarehe 19 July ikiwa imesheheni zawadi kibao kwa wateja wote ambao walitakiwa kununua simu ya Camon 17 au Spark 7.

Kila aliyenunua simu alipata zawadi za papo kwa hapo zikiwemo ear pods, Bluetooth Speakers, simu ndogo (vitochi) na zingine kibao. Wakati huo huo majina ya wateja hao yalikuwa yanaingizwa kwenye kapu la bahati kwa ajili ya kumpata mshindi wa mwisho ambaye angeibuka na gari mpya.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mshindi wa gari mpya Bi. Sophia Suleiman amesema kuwa “sina mengi zaidi ya kumshukuru Mwenyezi Mungu kwanza maana tulioshiriki ni wengi lakini mimi ndo mshindi, pili uongozi mzima wa kampuni yangu pendwa ya TECNO”

Bi. Suleiman amesema kuwa kiukweli yeye ni miongoni mwa watu ambao hawakuwa wakiamini katika haya mambo ya bahati nasibu kwani aliamini hivi vitu havipo, lakini nilishangaa sana kupokea sim una kuambiwa ni ndo mshindi.

“SIkutegema lakini ndo hivyo Mungu kaniona leo hii na mimi ni miongoni mwa wamiliki magari mjini hapa hivyo ni mwendo wa Kuvimba.”

Aliongeza kuwa “sijui kuendesha lakini so mda mrefu tukutane sheli kwenye foleni ya mafuta, kwa hiyo niwashauri Watanzania wenzangu wasipuuzie michezo hii ya bahati nasibu  maana kesho yaweza kuwa wewe ndo mshindi. Asante sana” amesema Bi. Suleiman

No comments