RC MAKALLA AVIAGIZA VYOMBO VYA USALAMA KUMKAMATA MWENYEKITI WA KAMPUNI YA ARDHI
Na John Luhende
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amosi Makalla ameviagiza vyombo ya usalama kumkamata Mwenyekiti wa kampuni ya Geolink Solution Tanzania LTD , Bwana Deogratius Kamugisha kwa tuhuma za kuwadhurumu wananchi katika zoezi la kupima ardhi mtaa wa Mbezi kati kata ya Mbezi Juu Wilayani Kinondoni.
Makalla ametoa AGIZO hilo Katika mkutano wa kusikiliza kero za wananchi Jimbo la Kawe baada ya wananchi walio dhurumiwa kutoa malalamuko yao.
Akizunguma katika mkutano huo Mwenyekiti wa mtaa wa Mbezi kati Frank mwanga amesema tangu ameingia madarakani yapata miaka miwili wananchi wamekuwa wako leta malalamuko yao nakwamba wamedhurumia zaidi ya Milion 18.
Makala yupo Katika ziara ya kusikiliza kero za wananchi Katika majimbo ya Pembezoni mkoani humo amabapo awali akizunguma Katika ufunguzi wa kutano huo amewataka wananchi wa majimbo yaliyolengwa Katika ziara hiyo kujitokeza kwa wingi Katika mikutano hiyo.
Post a Comment