MWENGE WA UHURU KUZINDUA MIRADI YA SHILINGI BILIONI 105 DAR
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla leo August 18 amepokea Mwenge wa Uhuru uliowasili asubuhi ya leo Uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere ukitokea Mkoa wa Pwani na kuukabidhi kwa Jiji la Ilala kwaajili ya kuanza shughuli ya uzinduzi na uwekaji mawe ya msingi kwenye miradi ya maendeleo.
Akipokea Mwenge huo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani Aboubakar Kunenge, RC Makalla amesema kwa siku tano ambazo Mwenge wa Uhuru utakuwa Dar es salaam utapitia miradi ya maendeleo 46 yenye thamani ya Shillingi Billion 105.1.
Mwenge wa Uhuru umeanza rasmi kukimbizwa leo Mkoa wa Dar es salaam kwa kuanzia Jiji la Ilala kisha katika Wilaya za Ubungo, Kinondoni, Kigamboni na Temeke ambapo ifikapo August 23 Mwenge huo utakabidhiwa kwa Mkoa wa Lindi ukienda na kaulimbiu inayolenga kuhimiza Matumizi sahihi ya TEHAMA.
Post a Comment