WAHITIMU CHUO CHA FURAHIKA WAPEWA MBINU KUFANIKIWA KIMAISHA
Afisa Vijana wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Masalida Zephania akizungumza jambo katika Mahafali ya tatu ya Chuo cha Furahika Education Centre yaliofanyika leo tarehe 10.4. 2021 jijini Dar es Salaam.
Naibu Mkuu wa Chuo Cha Furahika Education Centre Bw. David Msuya akizungumza jambo na waandishi wa habari leo tarehe 10. 4. 2021 kuhusu mahafali ya tatu ya chuo cha Furahika Education Centre kilichopo Buguruni jijini Dar es Salaam.
NA NOEL RUKUNUGA, DAR ES SALAAM.
Wahitimu wa Chuo cha Furahika Education Centre kilichopo Buguruni jijini Dar es Salaam wametakiwa kuwa wabunifu kwa kutumia taaluma zao vizuri jambo ambalo litasaidia kufanikiwa kimaendeleo pamoja na kuwa mabalozi wazuri.
Akizungumza katika mahafali ya tatu ya Chuo cha Furahika Education Center jijini Dar es Salaam, Afisa Vijana Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Masalida Zephania, amesema kuwa ni vizuri wahitimu kwa na malengo ambayo yatawasaidia kufikia mafanikio kwa kija jambo ambalo wamekusudia katika maisha yao.
Bw. Zephania ni mgeni rasmi katika mahafali hayo, amesema vijana wanatakiwa kuongeza jitihada katika kila jambo wanalofanya kwa kuzingatia taaluma zao katika kupambana na maisha.
"Mnastahili pongezi kubwa tunategemea mtayatendea haki maarifa haya kwa kufanya kazi kwa uweledi" amesema Bw. Zephania
Zephania amesema kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mama Samia Suluhu Hassani ipo pamoja na vijanai kwa kuwaandalia mazingira rafiki ya ajira kupitia viwanda vidogo vya kati na vikubwa.
Naibu Mkuu wa Chuo cha Furahika Education Centre Bw. David Msuya, amesema kuwa chuo kimeanzishwa kwa ajili ya kuwasaidia watoto wa kike kuondokana na changamoto mbalimbali ikiwemo kupata ujuzi utakaowawezesha kujikimu na maisha kwa kuondoa umasikini.
Amesema kuwa wanafunzi wanaomaliza mafunzo wamekuwa wakipata fursa za ajira kwenye maeneo tofauti ikiwemo kwenye makampuni, mahotelini, viwandani huku wengine wakijiajili wao wenyewe kupitia viwanda vidogo.
Mkuu huyo amewataka wahitimu kuzingatia misingi bora ya kazi, nidhamu na kujituma kwani ndio ngao pekee katika kufanikisha jitihada za maendeleo.
Rais wa serikali ya wanafunzi katika Chuo hicho Zainabu Adamu, amesema kuwa chuo cha Furahika kimewasaidia vijana wa kike kuondokana na mimba za utotoni kwa kupata mbinu mbadala za kukabiliana na changamoto za maisha.
Amesema kuwa mbali na kupata ujuzi chuo chao kimekuwa kikiwafundisha wanafunzi hao lugha mbalimbali ikiwemo kifaransa na kiingereza ili kuwawezesha kuwasiliana na watu kutoka mataifa mengine.
Ameeleza kuwa mbali na kupata ujuzi chuo chao kimekuwa kikiwafundisha wanafunzi hao lugha mbalimbali ikiwemo kifaransa na kiingereza ili kuwawezesha kuwasiliana na watu kutoka mataifa mbalimbali.
Furahika Education ni mradi ambao umelenga kuwasaidia vijana wa kike ambao unaoendeshwa chini ya usimamizi na udhamini wa watu kutoka nchini Ujerumani kwa kuwasaidia watoto wa kike kupata ujuzi wa kukabiliana na changamoto za maisha.
Wanaiunga mkono serikali ya Tanzania kuwawezesha watoto hao kufikia malengo kwa kuwapatia elimu bure.
Post a Comment