Bodi ya Wadhamini Mfuko wa Misitu yatoa neno ujenzi wa kiwanda cha mazao ya nyuki Wilaya Bukombe
Mfuko wa Misitu Tanzania unagharamia asilimia 95%, huku Halmashauri ya Wilaya Bukombe ikichangia asilimia 5% za ujenzi wa kiwanda hicho kitakachoendeshwa na Halmashauri ya Bukombe kwa mfumo wa Kampuni Tanzu (SPC).
Akizungumza wakati wa ukaguzi huo, Mwenyekiti wa
Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Misitu Tanzania, Prof Romanus Ishengoma amesifu
ujenzi unaoendelea na kuitaka Halmashauri kuwa ushirikiano wa karibu zaidi na TaFF.
Prof. Ishengoma aliongeza
kusema kwa kawaida tunapokuwa tumedhamini milioni 500 katika ujenzi wa kiwanda
kwa shughuli za nyuki mmoja ya changamoto ni upatikanaji wa malighafi.
“Utajiuliza je asali ipo tunaweza kuweka hapa
kiwanda cha milioni 500, fedha ya serikali tumeitumia. Uamuzi ni wa kwetu kama
bodi sasa kitakamilika ukajikuta unazunguka asali ipo wapi?”
Prof. Ishengoma anasema
“tumejiandaje kupata asali, nakumbuka kuwa tumewezesha vikundi vya ufugaji
nyuki lengo ni kufanya kiwanda hiki kama chachu, tunategemea sasa wilaya hii
ibue vikundi vingi zaidi.”
Katibu Tawala wa Mfuko wa
Misitu Tanzania (TaFF), Dkt Tuli Msuya amesema ni vema mchakato wa kuanzisha
kampuni tanzu uanza sasa kama lilivyosaini kwenye mkataba wa ujenzi wa kiwanda
hiki.
“Suala la kampuni Tanzu
siyo hiari kwa sababu tulisaini mkataba tukakubaliana kwamba tutaanzisha
kampuni tanzu ya kusimamia hichi kiwanda, ni vema tukaanza mchakato
tukapokamilisha ujenzi wa kiwanda kampuni inakuwa tayari ipo na inaanza kufanya
kazi.
Dkt Tuli amesema Mwenyekiti
anauzoefu atawaelezea umuhimu wa kampuni tanzu itakayosaidia uendeshaji wa
kiwanda.
Kamishna Mhifadhi Mkuu wa
Misitu (TFS), Prof Dos Santos Silayo amesema wilaya hii inasifika kwa kuzalisha
asali nzuri na taarifa zinaonyesha kuwa asali nyingi inayozalishwa hapa
inapelekwa nje na wafanyabiashara, si jambo baya kwa sababu ni mmonyororo mzima
wa biashara.
“Tujipange kupambana
kibiashara, tunatakiwa kuangali mazingira ya kibiashara ya kuifanya asali
isiende nje ikiwa ghafi bila ya kupita katika kiwanda hiki, hatuwezi kusema
asali ya Tanzania isiuzwe nje, lakini tunapambana nayo kibiashara.
Prof. Silayo anasema naamini
tutaanzisha kampuni tanzu itakayosimamia ufanyaji wa biashara wenye uwezo wa
kubadilika na kushindana na wengine, kwa sababu huwezi kumlazimisha mtu kuuza
bidhaa yake kwako kwa kuweka sheria za serikali.
“Tutakaponunua vifaa kwa
ajili ya kiwanda tuangalie vile ambavyo vitakuwa na uwezo wa kuchakata mazao
mbalimbali ya asali, tunakiwa kuwa makini na kutazama mbali,” Prof. Silayo.
Mapema Mkuu wa Wilaya ya
Bukombe, Said Nkumba amesema kutokana na maeneo yetu haya kuzungukwa na hifadhi
tumekuwana mazingira bora na salama ya kufuga nyuki wanaozalisha asali bora kwa
sababu ya kutokuwa na mwingiliano na shughuli za binadamu.
“Ujio wa kiwanda hiki
umekuja sehemu sahihi kwa sababu kitakuwa kiwanda endelevu kwa kuwa wakazi hapa
ni wafugaji nyuki hivyo kurahisisha upatikanaji wa malighafi.
Mhe. Nkumba amesema kiwanda
kile kitakapokuwa kimeanza ni muhimu kuwa na wataalamu wa kutosha katika
kukiendeleza kwa sababu hapa tuna afisa nyuki mmoja tu.
“Ili ufanisi uwepo ni
vizuri tukawa na watumishi watakaosaidia kuendeleza jambo kiwanda hiki na
kupata tija ya uwekezaji mkubwa uliofanywa hapa,” amesema Nkumba.
Naye Mkuu wa Wilaya ya
Temeke na mjumbe la Bodi TaFF, Mhe. Godwin Gondwe amesema ningependa mkurungezi
wa halmashauri ajue hiki ni kiwanda cha Serikali kwa lengo la kuongeza mapato
ya wilaya hii si cha mkuu wa Bodi TaFF.
“Ukiangalia jinsi ya
uchangiaji wa fedha za ujenzi utaona Halmashauri imetoa asilimia ndogo ya kile
wanachotakiwa kuchangia wakati Bodi imetoa zaidi ya asilimia 50 ya fedha zote
kwa hiyo commitment yao haionekani,” anasema Gondwe.
“Malighafi itakayotumika hapa wasiangalie ni Bukombe pekee wanatakiwa kutazama mkoa wote na mikoa ya jirani pia kutokana na ukubwa wa kiwanda chenyewe,” alisema Gondwe.
Post a Comment