Wananchi wapongeza TCRA kwa Watoa huduma za simu za mkononi kurudisha huduma ya bando ya awali.
Kufuatia hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Hassan Suluhu ya aliyoitoa katika uapishashaji wa Mawaziri na Kuitaka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuangalia upya vifurushi vya Bando, TCRA imekeleza kwa Watoa huduma za kampuni za simu ku kurudisha vifurushi vya Bando kuwa vya bei isiyomuumiza mwananchi limefanyika na kufanya wananchi kufurahia huduma hiyo.
Baada ya vifurushi kurejea na kufanya wananchi kuwa na uhakika wa kupata taarifa kwa njia ya mtandao pamoja na biashara kuendelea kufanyika kwa njia ya mtandao kwa kutoa maoni tofauti na kuipongeza Mamlaka hiyo.
Akizungumza kwa nyakati tofauti watumiaji wa vifurushi vya Bando la Internet wamesema kuwa maisha yalikuwa magumu kwao na huku baadhi wakishindwa kuendesha biashara kwa kutumia mtandao.
Mwanafunzi wa Chuo Cha Usafirishaji ( NIT) mwaka wa tatu Hamisi Mchuchuri amesema kuwa bando kuwa juu lilikuwa linawaathiri katika masomo kutokana maisha ya Chuo kuwa ya bajeti.
Amesema kuwa kuna vitabu vingine viko mtandaoni hivyo bila kuwa fedha zaidi ya 5000 huwezi kupata lakini sasa unapata hata sh.1000 na 2000 na kupata vifurushi vya kuweza kupakua vitabu vyote.
Mchuchuri amesema TCRA kupitia watoa huduma za simu wameweza kuboresha huduma za bando.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Uhamamasishaji wa Wanawake kutumia mitandao (TIBA) Marcela Lungu amesema kuwa kama wanaasasi walikuwa wanatumia fedha nyingi kwa ajili ya bando lakini sasa itapungua na kuweza kuwafikia wananchi kwa wakati.
Amesema wakati Ugonjwa wa Corona sehemu kubwa wanatumia mitandao kwa kununua bando kuendesha mikutano.
Kwa upannde wa Mjasirimali wa matunda Walter Hirispo amesema miasha ya bando kuwa juu yanaathiri watu wote hasa wenye kipato cha kuwaida kushindwa kumudu maisha hayo.
Naye Clemance Mtembela mfanyabiashara wa Duka Mtandao amesema kuwa biashara ya bando kurejea katika hali ya awali kumerahisha maisha kwa kuweza kuwafikia wateja wote kwa wakati na wakawa hewani.
Amesema wakati vifurushi vilivyokuwa juu baadhi ya watu walikuwa hawaingii mtandaoni kufanya biashara na hata wakiingia hawawezi kupakua huduma ndani ya mtandao
Post a Comment