Mchimbaji madini Dodoma aiomba Serikali iwapatie msaada kwenye mitaji na masoko.
Amesema kiliochao kikubwa kama mfanya biashara hiyo ni kuitaji serikali iwapatie sapoti kwenye mitaji na masoko .
Hayo yalisemwa na Samwel katika Maonesho ya Tume ya Madini yaliyoa malizika katikati ya wiki iliyo malizika Dar es Salaam kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC).
"Serikali isaidie kwa kuwapa sapoti ili kuchangia sekta hiyo wachimbaji kama yeye kuweza kusambaza tani nyingi zaidi na kuchangia kuleta tija kubwa kwa taifa," amesema Swamwel.
Samwel alisema akiwa ni mchimbaji mzalendo amesema mwaka jana alikuwa na hoda tani elfu kumi lakini alishindwa kusambaza kwa wakati .
Mchimbaji huyo wa madini ya Gypsum alisema wanaitaji serikali kuwawezesha kuwakopesha vifaa ili waweze kuchimba na kuwapelekea wateja kwa wakati .
Aidha Katika Mkutano huo ulioandaliwa na Wizara ya Madini uliohusisha wadau wa madini ikiwa ni pamoja na Taasisi za Serikali, Taasisi za Kifedha, kampuni za uchimbaji wa madini, wachimbaji wadogo wa madini, wafanyabiashara wa madini.
Alisema endapo serikali itampatia ya kumpatia magari ya kubebea mzigo kusafirisha kwenda nje ,serikali itaweza kujiingizia pato lake zaidi kupitia kodi.
Mchimbaji huyo ameshauri serikali kuijenga miundo mbinu imara kupitia wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini ( TARURA) .
"Barabara tunazotumia ni hizo zinazojengwa na TARURA ambapo huku katika eneo la kazi kumekuwa na madaraja yenye kushindwa kupitisha mzigo kwenda saiti na mzigo wakati wa kutoka saiti huko Maeneo ya Manda ,"alisema Samwel.
Alisema pia kumekuwa kunajitokeza hali ya kucheleweshewa malipo pindi wanapowauzia wafanya biashara wenye viwanda .
Mdau huyo wa ujimbaji madini ameendelea kuishukuru serikali kupitia kwa
Waziri wa madini Mh.Dotto Biteko ambapo ameeleza kuwa ameonesha juhudi kubwa na
nia ya kuwaonesha njia wadau hao katika kufikia malengo ya mafanikio.
Post a Comment