MANISPAA YA KIGAMBONI YAPATA MEYA
Msimamizi wa uchaguzi wa Meya Manispaa ya Kigamboni Dalmia Mikaya Tumaini ambaye ni katibu tawala wa Wilaya ya Kigamboni amemtangaza Ernest Mafimbo Ndamo Diwani wa Kata ya Tungu kuwa Meya wa Manispaa .
Mafimbo amechukua nafasi hiyo baadaya ya kupata kura zote 13 kati ya kura zilizopigwa na Madiwani wa kata tisa Mbunge na Madiwani watau wa viti maalumu, kwa upande wa Naibu Meya amechaguliwa Stephano Maganga Waryoba, naye kadhalika amepata kura zote 13 .
Akizungumza baada ya kuchaguliwa katika nafasi ya Mstahiki Meya Ernest Mafimbo amewataka Madiwani kufanya kazi kwa ushirikiano na watumishi wa Manispaa ili kuweza kutimiza majukumu yao ya kazi.
"Nashukuru kwa kunipa imani kubwa nami nawaahidi kuwa nitawatumikia pia nita tenda haki kwa madiwani wote bila ubaguzi wa aina yoyote ,tunaelekea hatua nyingine baraza lililopita lilikuwa makini likijadili mijadala kwa kuzingatia nguvu za hoja , niombe baraza hili tuuendeleze utamaduni huo"amesema.
Naye naibu meya Stephano Maganga Waryoba, akitoa salamu za shukrani amesema atakuwa mshauri mzuri kwa kwa viongozi na kuleta tija na atakuwa tayari kupokea maelekezo kutoka kwa viongozi wake.
Kabla ya uchaguzi huo Madiwani wateule wa Manispaa ya Kigamboni, walikula kiapo cha uaminifu na maadili , rasmi kwa kuanza kutekeleza majukumu yao ya uwakilishi wa wananchi Katika Manispaa na utekelezaji wa shuguli za Maendeleo.
Baada ya Meya na Naibu Meya kuongea na kutoa shukranizao Katibu Tawala alipata wasaa wa kuzungumza na madiwani hao ambapo amesema wananchi wamewaamini na serikali imewaamini amewataka kwenda kuwasikiliza na kutatua kero za wananchi kwa kuzingatia maslahi ya taifa na mkatenge siku zenu maalum hata maramoja kwa mwezi kukaa na kuzungumza na wananchi wenu .
"Waheshimiwa Madiwani mlio kula kiapo leo nawahidi kuwa tutashirikiana" Mikaya.
Post a Comment